Akizungumza na mtandao huu Magembe Makoya Katibu Mkuu wa chama hicho amesema kuwa migogoro ya wakulima na wafugaji kwa sasa yanachochewa na watumishi wa serikali wenye katika maeneo mbalimbali nchini.Amesema kuwa mfululizo matukio yaliyotokea katika jamii hizo siku za karibuni yaliyofanywa na watendaji wa serikali pamoja na jeshi la Polisi yanawaonea jamii ya wafugaji na yapo kinyume cha sheria za nchi.
Katibu huyo amemtaja Alhaji Majjid Mwanga Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo kuwa amekuwa kinara wa kuchochea migogoro kati ya wafugaji na jamii nyengine ambapo yeye amekuwa akihubiri kutendea uovu wafugaji kutokana kwa madai ya kwamba wafugaji hao si wakaazi wa wilaya hiyo.
Makoye ameeleza Mkuu wa wilaya huyo alinukuliwa katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika maeneo ya Miono, Mkwajuni na Namba nne Novemba mwaka jana ambapo alisisitiza kuwa wafugaji wafanywe vyovyote.
“Mkuu wa wilaya anathubutu kusema Maneno hayo hadharani unafikiri kuwa ataweza kutatua migogoro hiyo” amesema Makoye.
Ametaja tukio liliotokea tarehe 16 Agosti mwaka ambapo jeshi la Polisi wilayani humo linatuhumiwa kumuua kwa kumpiga risasi za mfugaji Gegona Lughumeda Molanu.
Amedai kuwa walimuokota mtu yule na kumpelekea Hospital ambapo alifanyiwa uchunguzi na kubainika kuwa amepigwa risasi.
Makoya ameeleza kuwa utata wa kifo hicho umepelekea Mkuu wa Mkoa wa Pwani kuunda kamati ya Uchunguzi itakayochunguza maauaji hayo.
Katika mkutano huo Makoye ameweka bayana kuwa wafugaji wanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo, wafugaji kuuawa, mifugo kuuawa, kutozwa faini kubwa, na kutowekewa bayana maeneo ya kufugia, na baadhi ya watendaji wa serikali wakiwemo madiwani wanaowaona wachungaji kama chanzo cha mapato, badala ya kuwasaidia katika matatizo yanayowakabili.
Wafugaji wamemtaka rais dk John Magufuli kuwasaidia kwa kuingilia kati kutambua kuwa nao ni watanzania, wanafukuzwa bila kuelekezwa wapi waende hali inayosababisha waishi kama wakimbizi katika nchi yao.
0 comments:
Post a Comment