Home » » Somalia: afisa mwandamizi wa jeshi auawa mjini Mogadishu

Somalia: afisa mwandamizi wa jeshi auawa mjini Mogadishu

    media
    Wanajeshi wa Somalia wakipiga kambi mbele ya hoteli ya Maka al-Mukarama ambayo ilishambuliwa na wapiganaji wa Al Shabab, mjini Mogadiscio, Machi 28, 2015.
    Afisa mwaandamizi na walinzi wake wanne wameuawa Jumapili hii Septemba 18 mjini Mogadishu, nchini Somalia katika shambulizi la kujitoa mhanga linalodaiwa na kundi la wanamgambo wa Kiislam la Al Shebab.
    Gari "lililokua limejaa mabomu liligongana na lori la kijeshi kando ya barabara" na kusababisha vifo vya "askari wengi, ikiwa ni pamoja na afisa mwaandamizi mwenye cheo cha juu," kulingana na chanzo cha polisi.
    Shambulizi hilo liliolomuua Jenerali Mohamed Jimale Goobaale na walinzi wake wanne lililotokea karibu na makao makuu ya jeshi.
    Jimale alikuwa amenusurika majaribio mengi ya kumuua, ambayo yamekua yaliendeshwa na wanamgambo wa kundi la Al Shabab.
    Wapiganaji wa kundi la Al Shabab wamekiri kutekeleza shambulizi hili wakisema kuwa jenerali huyo alikuwa akipanga na kutekeleza mashambulizi mengi dhidi yao.
    Nchi ya Somalia imeendelea kukumbwa na mashambulizi mbalimbali yanayolenga wanajeshi, askari polisi na maafisa mbalimbali wa serikali. RFI

    Tuma Maoni



    Toa maoni yako kwa habari hii kwa kuweka email yako hapa,na endelea kutufatilia zaidi Ukurasa wa habari

    0 comments:

     
    Supported by AMAGA Media services : | |
    Copyright © 2015. UKURASA WA HABARI - All Rights Reserved
    Templete Designed by Abdallah Magana
    Proudly powered by Blogger