Jumapili ya Septemba 18 2016 klabu ya Man United ilishuka dimbani kucheza mchezo wake wa tano wa Ligi Kuu England dhidi ya Watford ambao walikuwa wenyeji wa mchezo huo, Man United wakiwa ugenini waliruhusu kufungwa magoli 3-1 na huo kuwa mchezo wao wa tatu mfululizo kupoteza.
Baada ya kupoteza mchezo huo ambao ulikuwa wa tatu baada ya kupoteza dhidi ya Man City katika dimba la Old Trafford kwa goli 2-1 na kupoteza dhidi ya Feyenoord katika mchezo wa Europa League kwa goli 1-0, presha mitandaoni iliendelea kumuandama Paul Pogba aliyenunuliwa kwa dau kubwa na kuweka rekodi ya usajili.
Kiungo huyo wa Ufaransa ambaye hajafanya vizuri bado akiwa na Man United toka avunje rekodi ya usajili alitumia account yake rasmi ya instagram kuandika ujumbe kwa mashabiki
“Asante kwa mashabiki wote kuwa pamoja na sisi matokeo bado sio mazuri
kwa upande wetu, lakini tunaendelea kupambana, Man United tunaweza”
0 comments:
Post a Comment