“Tumecheza vizuri sana, tuliruhusu goli kwasababu tuliacha kucheza. Tulikuwa na hofu na tulipofanya mabadiliko kila kitu kikawa shwari, ni kitu ambacho tunapaswa kufanyia kazi.
“Kimsingi siangalii sana haya matokeo lakini naangalia namna gani tumecheza. Tumekuwa tukiimarika siku hadi siku kwa kiwango kikubwa.”
Alipoulizwa kama anaweza kukaa meza moja na Mourinho na kupata kinywaji, Mazzarri ambaye wakati yuko Napoli aliwahi kukwaruzana na Mourinho wakati yuko Inter Milan alisema: “Kama ana muda basi sina tatizo tutatekeleza hilo. Kabla ya mechi tulizungumza, hata ikitokea siku yoyote wiki ijayo ikapatikana nafasi basi tutapata wote kwa pamoja chakula cha usiku.”
Bosi wa Manchester United Mourinho: “Nimepata mambo matatu kutoka kwenye mchezo huu, lakini moja tu kati ya hayo yote naweza kurekebisha.
“Sababu ya kwanza kutokana na makosa yetu wenyewe, inahusisha makosa ya mtu mmoja mmoja na ya kitimu kwa maana ya mchezaji mmoja-mmoja na timu kwa ujumla. Lazima tuhakikishe tunafanya marekebisho ili kuimarika, suala hilo liko mikononi mwetu.
“Sababu ya pili ni mwamuzi na siwezi kuvumilia kunyamazia makosa yao.
“Sababu ya tatu ni bahati, hatukuwa na bahati. Wakati tunafungwa mchezo huu sisi ndio tulikuwa timu bora.”
0 comments:
Post a Comment