Waandamanaji
wameweka vizuizi na kuchoma magari katika mji mkuu wa Kinshasa nchini
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo,baada ya maafisa wa polisi kuwazuia
kuandamana.
Wanamtaka rais Joseph Kabila ajiuzulu baada ya
kukamilika kwa muhula wake mnamo mwezi Disemba tarehe 20 kulingana na
mwandishi wa BBC Poly Muzalia.Chombo cha habari cha reuters kiliwanukuu mashahidi wakisema kuwa maafisa wa polisi walifyatua risasi kuwatawanya waandamanaji.
Upinzani unahofia kwamba bwana Kabila ana mpango wa kuchelewesha uchaguzi wa urais unaotarajiwa mwezi Novemba ili kusalia madarakani.
Maafisa wa uchaguzi na serikali wanasema kuwa uchaguzi huo utaahirishwa kutokana na matatizo ya mipango katika taifa hilo la Afrika ya kati.
Taifa la DRC halijawahi kuwa na ukabidhi wa mamlaka ulio huru tangu uhuru wake zaidi ya miaka 45 iliopita.
0 comments:
Post a Comment