Kituo cha habari cha Uingereza BBC kimemtaja nyota wa timu ya taifa ya Algeria Yacine Brahimi kuwa mchezaji bora wa Afrika kwa mwaka 2014.
Brahimi ambaye anachezea klabu ya Ureno ya Fc Porto anakuwa raia wa kwanza wa Algeria kutwaa tuzo hiyo ambayo hutolewa na BBC kila mwaka .
Brahimi ametwaa tuzo hii kufuatia uwezo aliouonyesha kwa mwaka huu akiwa na timu yake ya taifa hasa kwenye michuano ya kombe la dunia ambako Algeria walifanikiwa kufika hatua ya 16 bora .
BBC imekuwa na utaratibu wa kuandaa tuzo hizi kila mwaka ambapo kwa miaka miwili iliyopita kiungo wa Ivory Coast Yaya Toure amekuwa akitawala .
0 comments:
Post a Comment