Akizungumza mara baada ya kuisaini mkataba huo kwenye ofisi za timu zilizopo jengo la Mkapa Hall jijini Mbeya, Nyoso aliyewahi kucheza kwenye timu za Ashanti United, Simba na Coastal Union, alisema amekubari kujiunga na City kwa mkataba wa mwaka mmoja kwa imani kuwa utatosha kuushawishi uongozi wa timu kumpa mkataba mrefu zaidi mara baada ya huu wa sasa.
“City ni timu nzuri na imekuwa hivyo toka ilipoanzishwa miaka minne iliyopita, matokeo yaliyoo sasa ni sehemu ya soka ambayo timu yoyote inaweza kuyapata, nimekubari kujiunga na timu kwa mkataba wa mwaka mmoja kwa sababu naamini uwezo wangu uwanjani utawashawishi viongozi kunipa mkataba mrefu zaidi pindi huu utakapo malizika na nina amini hili linawezekana kwa sababu nataka kukaa kwenye timu hii mpaka mpira wangu utakapoisha” alisema Nyosso
Akiendelea zaidi beki huyo aliyewahi pia kucheza kwenye kikosi cha timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ alisema kuwa mafanikio iliyopata Mbeya City msimu uliopita yamekuwa sababu kubwa ya yeye kukubari kujiunga na City huku akiamini kuwa amekuja kuongeza nguvu kwenye timu bora ili kuhakikisha mafanikio ya msimu uliopita yanafanikiwa tena.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa City Emmanuel Kimbe alimshukuru Nyosso kwa kukubari kujiunga na timu hii huku akiamini kuwa uzoefu alionao mchezaji huyo utasaidia kuimarisha safu ya ulinzi kwenye kikosi cha City.
“Tunamshukuru kukubari kujiunga nasi, imani yetu kubwa kwamba uzoefu alionao utasaidia kuimarisha safu yetu ya ulinzi, hasa ukizingatia matokeo tuliyopata katika michezo saba ya mwanzo wa Ligi hii” alisema Kimbe huku kauli yake hiyo ikiungwa mkono na Kocha Mkuu Juma Mwambusi.
Kwa sasa Nyosso tayari yuko na kikosi cha City kilichosafiri kwenda mjini Songea kwa ajiri ya michezo ya kirafiki
1 comments:
dah safi sana naamini timu itaimalika sana pongezi kwa vikongozi wetu wa MCC FC
Post a Comment