Home »
» WAKAZI WA KIZWITWE MKOANI RUKWA WACHOMA MOTO OFISI ZA KATA BAADA YA KUCHELEWESHWA KUPIGA KURA
WAKAZI WA KIZWITWE MKOANI RUKWA WACHOMA MOTO OFISI ZA KATA BAADA YA KUCHELEWESHWA KUPIGA KURA
Wakazi wa kata ya kizwitwe wilayani Sumbawanga mjini Mkoani Rukwa wamechoma moto ofisi za kata hiyo baada ya kucheleweshwa kupiga kura.
Ikiwa ni siku ya kuchagua viongozi wa mabaraza nchini Tanzani,Hali imekuwa tete Mkoani Rukwa baada ya wananchi kuchereweshwa kupiga katika maeneo mbalimbali mkoani hapa na baadhi ya maeneo kuhairishwa kabisa kwa uchaguzi huu.
Hayo yanatokea baada ya wananchi kuambiwa uchaguzi utaanza mida ya saa 2 asubhui lakini kufika mpaka majira ya saa 7 mchana vifaa vya kupigia kura vilikua bado avijafika,
Kutokana na hali hiyo wananchi wa kata ya kizwitwe wakachukua hatua ya kubomoa na kuchoma moto ofisi ya kata baada ya kusubiri kwa muda mrefu vifaa hivyo vya kupigia kura.
Taarifa zaidi hapo baadae kwani hali ni tete maeneo haya ya kizwitwe hapa wilayani Sumbawanga kwani mabomu ya machozi yanalindima
0 comments:
Post a Comment