Ufisadi nchini Kenya bado uko katika kiwango cha juu licha ya juhudi kukabiliana na swala hilo nyeti.
Sufuri ina maanisha kwamba ufisadi umekithiri huku na 100 ikionyesha kwamba taifa hilo halina ufisadi.
Hatahivyo ni taifa la Burundi lenye ufisadi mkubwa miongoni mwa mataifa ya Afrika mashariki likifuatiwa na Uganda na baadaye Kenya kulingana na utafiti huo.
Kulingana na mkurugenzi wa shirika hilo nchini Kenya Samuel Kimeu,Kenya haijabadilika katika nafasi yake tangu mwaka 2012.
Amesema kuwa taasisi za umma zinahitajika kuwa wazi kuhusu maamuzi yao .
Katika afrika mashariki ,ni taifa la Rwanda Pekee ambalo limeonyesha juhudi za kukabiliana na ufisadi.
Rwanda imeorodheshwa ya 49 ikiwa na alama 54,Ushelisheli iko katika nafasi ya 47 ikiwa na alama 54 na Mauritius ikiwa katika nafasi ya 52 ikiwa na alama 52 ikitamatisha mataifa matano bora barani Afrika.
Botswana imesalia kuwa taifa ambalo halina ufisadi barani Afrika likiwa katika nafasi ya 30 na alama 64 likifuatiwa na Cape Verde ilio katika nafasi ya 41 na alama 58.Baadhi ya mataifa yalio na ufisadi duniani ni Somali,Sudan,Sudan Kusini Libya na Guinea Bissau.
0 comments:
Post a Comment