.
Viongozi wa kitaifa wa wafanyabiashara nchini.
Baadhi ya wafanyabiashara walio udhuria mkutano jiji Mbeya.
Jumuiya ya wafanyabiashara nchini imewataka viongozi wa serikali wanaosimamia sekta ya biashara nchini kufanya kazi kwa kushirikisha na wafanyabiashara ili kusaidia kukuza kiwango cha uchumi nchini.
Rai hiyo imetolewa na mwenyekiti wa jumuiya ya wafanyabiashara nchini Ndg Johnson Minja katika mkutano mkuu taifa wa wafanyabiashara nchini uliowashirikisha wafanyabiashara kutoka mikoa mbalimbali nchini.
Mkutano huo uliofanyika jijini Mbeya ,Minja alisema mataifa makubwa yaliyoendelea kiuchumi duniani ni kutokana na sera nzuri inayozingatia hali halisi ya wananchi ambapo amedai kuwa uchumi wa nchi hujengwa na wafanyabiashara
Hata hivyo ameiomba serikali inapofanya maamuzi juu ya wafanyabiashara iwashirikishe wahusika na wadau ambao ni wafanyabiashara ili kuepuka migogoro inayoweza kujitokeza baina ya pande hizo mbili.
Aidha amesema kuwa mgogoro uliopo baina ya wafanyabiashara na serikali ni kuhusu mashine za kutolea stakabadhi (EFD) ambapo amedai kuwa mashine hizo ni kandamizi kwa wafanyabiashara jambo linalopelekea wafanyabiashara kufunga maduka mara kwa mara hali inayochangia kushuka kwa uchumi wa wafanyabiashara kwa ujumla,Pia ameitaka serikali kuliangalia upya suala hilo kwani linamgusa kila mtu na sio wafanyabiashara pekee.
Sanjari na hayo kueleke katika uchaguzi wa viongozi Minja amewataka wafanyabiashara na watanzania kwa ujumla kuchagua viongozi waadilifu na sio viongozi wanaoingia madarakani kwa maslahi yao binafsi.
Pia viongozi wawakilishi wa wafanyabiashara kutoka mikoani wamesema mashine za EFD zimekuwa changamoto kwa wafanyabiashara kwani hawana uelewa wa kutosha kuhusu mashine hizo.
Mkutano huo uliofanyika jijini Mbeya katika ukumbi wa Mkapa conference ulikuwa na lengo la kutoa elimu kwa wafanyabiashara na kutetea haki zao.
Na.Emmanuel Aswile Mwinuka.
0 comments:
Post a Comment