MATOKEO YA ASTON VILLA NA MANCHESTER UNITED YAPO HAPA



 Photo: Goal! Villa 1 United 1 (53'). Radamel Falcao's great header levels the score at Villa Park. That’s more like it!
Kikosi cha kocha Luis Van Gaal Kimelazimishwa sare ya goli 1-1 dhidi ya Aston villa katika uwanja wa Villa Park.

Photo: HT: Villa 1 United 0. The Reds have shown promise away from home but must now turn possession into goals after Christian Benteke’s opener. 

Will Louis van Gaal change tactics for the second half?

Aston Villa walikuwa wakwanza kupata goli dakika ya 23 kipindi cha kwanza lakini dakika ya 53 kipindi cha pili Ramadel Falco alisawazisha goli na mpaka dakika 90 zinakamilika Aston Villa 1-1 Manchester United, kwa matokeo hayo Man united wanafikisha point 32  wakiwa nafasi ya 3 nyuma ya Chelsea na Man City.

Izzo Bizness - Walalahoi (Official Video)

JCB Kijiti 2

RATIBA YA WIKIENDI HII YA LIGI KUU ENGLAND HIPO HAPA


Premier League
Premier League fixture



    Team 1 Score Team 2
    Saturday 20 December


    Manchester City 04:45 Crystal Palace

    Aston Villa 07:00 Manchester United


    Hull 07:00 Swansea


    QPR 07:00 West Bromwich


    Southampton 07:00 Everton


    Tottenham 07:00 Burnley


    West Ham 07:00 Leicester
    Sunday 21 December


    Newcastle 05:30 Sunderland


    Liverpool 08:00 Arsenal
    Monday 22 December


    Stoke 12:00 Chelsea

    CHADEMA YAPATA PIGO GEITA,MSHINDI WA SERIKALI ZA MITAA AKUTWA AMEFARIKI



      

    Chama cha democrasia na maendeleo mkoani Geita kimepata pigo baada ya mshindi wa serikali za mitaa Bertha Chimani, kukutwa amefariki katika shimo la choo.


    Chanzo;Nipashe

    MANCHESTER UNITED YAICHAPA 3-0 LIVERPOOL




    Magoli ya Wayne Rooney,Juan Mata na Van Parsie yameipa ushindi Manchester United wa magoli 3-0 dhidi ya mahasimu wao wakubwa Liverpool.





    Photo: Goal! United 3 Liverpool 0 (71’) – Juan Mata rolls the ball right for Robin van Persie to steer into an empty net with Brad Jones stranded.                                                   
    Kwa ushindi huo Manchester united wamefikisha pointi 31 wakiwa nyuma kwa pointi  8 dhidi ya vinara Chelsea ambao wana pointi 39, wakifuatiwa na Manchester City wenye pointi 36 wakiwa katika nafasi ya pili na nafasi ya tatu ikishikwa na mashetani wekundu Man u



    WAKAZI WA KIZWITWE MKOANI RUKWA WACHOMA MOTO OFISI ZA KATA BAADA YA KUCHELEWESHWA KUPIGA KURA








    news inscription in studio tv                                                                         
    Wakazi wa kata ya kizwitwe wilayani Sumbawanga mjini Mkoani Rukwa wamechoma moto ofisi za kata hiyo baada ya kucheleweshwa kupiga kura.

    Ikiwa ni siku ya kuchagua viongozi wa mabaraza nchini Tanzani,Hali imekuwa tete Mkoani Rukwa baada ya wananchi kuchereweshwa kupiga katika maeneo mbalimbali mkoani hapa na baadhi ya maeneo kuhairishwa kabisa kwa uchaguzi huu.

    Hayo yanatokea baada ya wananchi kuambiwa uchaguzi utaanza mida ya saa  2 asubhui lakini kufika mpaka majira ya saa 7 mchana vifaa vya kupigia kura vilikua bado avijafika,

    Kutokana na hali hiyo wananchi wa kata ya kizwitwe wakachukua hatua ya kubomoa na kuchoma moto ofisi ya kata baada ya kusubiri kwa muda mrefu vifaa hivyo vya kupigia kura.

    Taarifa zaidi hapo baadae kwani hali ni tete maeneo haya ya kizwitwe hapa wilayani Sumbawanga kwani mabomu ya machozi yanalindima

    WAFANYABIASHARA NCHINI WAITAKA SERIKALI KUANGALIA UPYA SUALA LA MASHINE ZA EFD.






     .






    Viongozi wa kitaifa wa wafanyabiashara nchini.













    Baadhi ya wafanyabiashara walio udhuria mkutano jiji Mbeya.
    Jumuiya  ya wafanyabiashara nchini imewataka viongozi wa serikali wanaosimamia sekta ya biashara  nchini kufanya kazi kwa kushirikisha na wafanyabiashara ili kusaidia kukuza kiwango cha uchumi nchini.

    Rai hiyo imetolewa na mwenyekiti wa jumuiya ya wafanyabiashara nchini Ndg Johnson Minja katika mkutano mkuu taifa wa wafanyabiashara nchini uliowashirikisha wafanyabiashara kutoka mikoa mbalimbali nchini.

    Mkutano huo uliofanyika jijini Mbeya ,Minja alisema mataifa makubwa yaliyoendelea kiuchumi duniani ni kutokana na sera nzuri inayozingatia hali halisi ya wananchi ambapo amedai kuwa uchumi wa nchi hujengwa na wafanyabiashara

    Hata hivyo ameiomba serikali inapofanya maamuzi juu ya wafanyabiashara iwashirikishe wahusika na wadau ambao ni wafanyabiashara ili kuepuka migogoro inayoweza kujitokeza baina ya pande hizo mbili.

    Aidha amesema kuwa mgogoro uliopo baina ya wafanyabiashara na serikali ni kuhusu mashine za kutolea stakabadhi (EFD) ambapo amedai kuwa mashine hizo ni kandamizi kwa wafanyabiashara jambo linalopelekea wafanyabiashara kufunga maduka mara kwa mara hali inayochangia kushuka kwa uchumi wa wafanyabiashara kwa ujumla,Pia ameitaka serikali kuliangalia upya suala hilo kwani linamgusa kila mtu na sio wafanyabiashara pekee.

    Sanjari na hayo kueleke katika uchaguzi wa viongozi Minja amewataka wafanyabiashara na watanzania kwa ujumla kuchagua viongozi waadilifu na sio viongozi wanaoingia madarakani kwa maslahi yao binafsi.

    Pia viongozi wawakilishi wa wafanyabiashara kutoka mikoani wamesema mashine za EFD zimekuwa changamoto kwa wafanyabiashara kwani hawana uelewa wa kutosha kuhusu mashine hizo.

    Mkutano huo uliofanyika jijini Mbeya katika ukumbi wa Mkapa conference ulikuwa na lengo la kutoa elimu kwa wafanyabiashara na kutetea haki zao.  

    Na.Emmanuel Aswile Mwinuka.








































    WANAHARAKATI NCHINI KENYA WATUMIA PUNDA KUFIKISHA UJUMBE KWA SERIKALI

     
    TZA-PUNDA WENYE GRAFITTI

    Kenya ni moja ya nchi ambazo huwa zinakaa kwenye headlines ya kuwa na story kubwa Afrika Mashariki, ya leo inahusu punda waliobebeshwa ujumbe maalumu na kuachwa katikati ya jiji la Nairobi.
    Desemba 11 katikati ya jiji la Nairobi katika moja ya barabara zenye shughuli nyingi ya Moi, lori moja lilisimama na kushusha punda wapatao 22 walio na maandishi yenye ujumbeTumechoka”.
    TZA-UJUMBE WA PUNDA



    Wanaharakati nchini Kenya wametajwa kuhusika na hii ambapo pia wamewahi kutumia njia mbalimbali ili kufikisha ujumbe wao ambapo moja ya waliyowahi kuifanya ni ile ya kuyabeba majeneza idadi sawa na Wabunge.

    Taarifa zinasema kuwa huu mtindo wa kuwashirikisha wanyama kwenye maandamano ya kudai haki ilianzishwa na mwanaharakati ambaye pia ni mkurugenzi wa Pawa 254, Boniface Mwangi japo safari hii haijafahamika sababu ya kuwatumia wanyama hao kufikisha ujumbe huo.

    Tumechoshwa na uongozi mbaya… ” alisikika mmoja ya wanaharakati huku akiwasukuma punda hao kutoka nje ya Lori.

    Polisi wanasema wanawasaka wale waliohusika na kitendo hicho.

    TZA-WANANCHI WAKISTAAJABU PUNDA WENYE GRAFITTI
    TZA-UJUMBE WA PUNDA
    141211133827_donkeys_7 (1)

    MAGAZETI YA LEO JUMANNE HAYA HAPA


    1_copy_f6d98.jpg
    2_copy_fba64.jpg
    3_copy_7d0ab.jpg
    4_copy_ebaf1.jpg
    5_copy_c73bc.jpg
    6_copy_61020.jpg
    7_copy_14910.jpg
    8_copy_60db3.jpg
    9_copy_b16ff.jpg
    11_copy_b4742.jpg
    20_copy_5a59b.jpg
    21_copy_f3416.jpg
    22_copy_0eb98.jpg
    23_copy_e9824.jpg
    24_copy_70e40.jpg
    25_copy_69542.jpg
    26_copy_eabce.jpg
    27_copy_d7a83.jpg
    28_copy_ddb54.jpg
    29_copy_1ed79.jpg
    30_copy_17569.jpg
    31_copy_e9706.jpg
    40_copy_2e704.jpg
    42_copy_b6bd7.jpg
    43_copy_38df1.jpg

      27_copy_d7a83.jpg

     44_copy_ca665.jpg

     

     Chanzo; Mjengwa blog 


     
    Supported by AMAGA Media services : | |
    Copyright © 2015. UKURASA WA HABARI - All Rights Reserved
    Templete Designed by Abdallah Magana
    Proudly powered by Blogger