UPDATE:EUROPA LEAGUE


Rais Magufuli ametengua tena uteuzi wa mtendaji mwingine wa Serikali

u
April 14 2016 imetolewa taarifa kutoka Ikulu na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi ikieleza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mhariri mtendaji  wa magazeti ya serikali ‘TSN’, Gabriel Nderumaki.
Rais Magufuli ametengua uteuzi huo kuanzia March 18 2016, kufuatia kutenguliwa kwa uteuzi huo, Rais Magufuli amemteua Tuma Abdallah kukaimu nafasi hiyo ambapo Tuma Abdallah ni Mhariri Mtendaji Msaidizi wa Magazeti ya Serikali ‘TSN’.
ikulu
 

Hakielimu yashauri bajeti ya Elimu 2016/2017

Wanafunzi wakiwa katika shule iliyokuwa katika mazingira magumu
Wanafunzi wakiwa katika shule iliyokuwa katika mazingira magumu

  KATIKA kuelekea bunge la bajeti hivi karibuni, serikali imeshauriwa kuongeza bajeti ya sekta ya elimu kwa mwaka wa fedha 2016/2017 ili kuendana na kauli ya upatikanaji wa elimu bure sambamba na kufidia gharama za uboreshaji na ujenzi wa miundombinu, 

Kauli hiyo imetolewa leo Jijini hapa na John Kalage Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Hakielimu, wakati alipokuwa akitoa taarifa ya uchambuzi na ushauri wa Shirika la Hakieli juu ya mwelekeo wa bajeti ya elimu2016/2017.
Kalaghe amesema serikali haina budi kuongeza bajeti ya sekta ya elimu kwa mwaka wa fedha 2016/2017 hadi kufikia asilimia 20 ya bajeti ya taifa au asilimia 6 ya pato lote la taiafa.
Aidha amesema kwa mujibu wa uchambuzi walioufanya kama shirika, na kwa kuzingatia takwimu za idadi ya wanafunzi, shule na mahitaji, kila mwaka serikali itapaswa kutenga kiasi cha fedha kisichopungua Tsh. bilioni 1,034.5 nje ya mahitaji mengine ya kisekta ili kugharamia elimu bila malipo.
“Tunafahamu hivi karibuni bunge linatarajiwa kuanza vikao vyake na kama watetezi na mdau wa upatikanaji wa elimu bora nchini, tunapendekeza kwa serikali maeneo ambayo yanahitaji kutiliwa mkazo katika upangaji wa bajeti ya sekta ya elimu yazingatiwe” amesema Kalage.
Akizungumzia maeneo muhimu ambayo serikali inatakiwa kuyazingatia katika upangaji wake wa bajeti kupitia sekta hiyo amesema ni pamoja na eneo la bajeti ya utekelezaji wa elimu bila ada, upangaji wa bajeti ya sekta ya elimu, bajeti ya ukaguzi na uhakiki wa ubora wa elimu, mwongozo wa sera ya mpya ya elimu na makadirio bajeti ya sekta ya elimu 2016/2017.
Amebainisha kuwa eneo la bajeti ya utekelezaji wa elimu bila ada, linapaswa kuanza kutekelezwa kabla ya agizo la elimu bila ada, suala hilo lilikuwa likitekelezwa kupitia michango ya wazazi kwa kuchangia elimu kwa kushirikiana na serikali.
Aidha kuhusu gharama za kufidia ada na ruzuku shuleni kwaajili ya vifaa, gharama za mitihani na gharama za uendeshaji kwa shule za msingi na sekondari amesema, kwa kuwa gharama hizo zilikuwa zikifanikishwa awali kwa ushirikiano wa michango ya wazazi na serikali basi serikali inapaswa kufidia gharama zote kwa kutenga kiasi cha sh.bilioni 161.5 katika maeneo hayo.
Akielezea gharama za kufidia ujenzi na miundombinu ambao nao ulikuwa ukichangiwa na wazazi alisema serikali kufidia gharama hizo kwa kutenga bilioni 1, 438 huku kwa upande wa gharama za kufidia utoaji wa uji katika shule za msingi na awali itenge kiasi cha sh 198.
Vile vile kuhusu upangaji wa bajeti wa sekta ya elimu, ameshauri kuwa licha ya changamoto zilizopo katika upangaji wa matumizi katika sekta ya elimu, serikali inatakiwa kuangalia namna ya kuweka uwiano wa bajeti ya matumizi ya kawaida na ya maendeleo.
“Tunaona katika kipindi cha miaka mitano iliyopita wastani wa bajeti ya maendeleo ya sekta ya elimu imekuwa kati ya asilimia 11 hadi 16 tu wakati ile ya matumizi ya kawaida ikifikia asilimia 80 hadi 90, kihalali kiasi kinachotengwa ni kidogosana kulinganisha na changamoto,
“Mathalani bajeti ya mwaka 20215/2016 bajeti nzima ilikuwa sh. Bilioni 3,887 huku bajeti ya maendeleo ikiwa ni asilimia 16 tu” amesema.

Upinzani waandamana Zimbabwe


Image caption Kiongozi wa MDC Morgan Tsvangirai
Karibu wafuasi 2000 wa upinzani nchini Zimbabwe wamekuwa wakifanya maandamano katika mji mkuu Harare, kulalamikia kuendelea kuzorota kwa uchumi wa nchi hiyo.
Waandamanaji hao waliongozwa na kiongozi wa chama cha (Movement for Democratic Change) Morgan Tsvangirai.
 
Image caption Waandamanaji wanalalamikia kuzorota kwa uchumi wa nchi hiyo.
Wengi walibeba mabango wakimtaka rais wa Zimbabwe Robert Mugabe , mwenye umri wa miaka 92 ajiuzulu.
Polisi wa kupambana na ghasia walifunga barabara za kuelekea majengo ya bunge ya nchi hiyo.

Utafiti: Vijana wengi Tanzania hawafanyi kazi

Uchunguzi Ruth


  Utafiti huo uliangazia mwaka 2014/2015

Utafiti umebaini kwamba asilimia 71 ya Watanzania wenye umri kuanzia miaka 15 hadi 35 wanatumia muda wao mwingi kwenye shughuli zisizo za uzalishaji mali.
Badala yake hutumia muda huo kujihudumia kwenye gesti, baa, kulala na katika shughuli za starehe.
Serikali imesema hali hii inaichelewesha Tanzania kuingia katika kundi la mataifa yenye uchumi wa kati kufikia mwaka 2025.
Bi Ruth Minja, ambaye ni mtakwimu mkuu katika ofisi ya taifa ya takwimu Tanzania, ndiye aliyeongoza utafiti huo wa watu wenye uwezo wa kufanya kazi kwa mwaka 2014/2015.



 
Uchunguzi
  Ripoti ya uchunguzi huo imezinduliwa leo Dar es Salaam
Anasema waligundua kuwa watu wenye uwezo wa kufanya kazi walikuwa milioni 25 kutokana na kiashiria cha saa za kufanya kazi kupungua na baadhi ya wafanyakazi kupunguzwa kazi kutokana na utendaji dhaifu.
Ally Msaki, aliyemuwakilisha katibu mkuu katika ofisi ya waziri mkuu anayeshughulikia masuala ya kazi,vijana ajira na watu wenye ulemavu amewaangazia Watanzania walioko kwenye ajira, ambao wanapata kipato ambacho hakitoshelezi kuweza kumudu gharama za maisha.
Amesema nafasi kama hizo za kazi hazina viwango vya ubora na ni kinyume cha maelekezo ya shirika la wafanya kazi duniani ILO.
Ingawa Sera ya taifa ya ajira kwa Taifa la Tanzania kwa mwaka 2008 ilijikita zaidi katika kuongeza fursa za ajira na kufanikiwa katika lengo lake, kuna kasoro kwenye kipengele cha ubora wa ajira.

Waziri Mkuu 'aliyehudumu' siku mbili Australia



Aliyesingizia utajiri kukwepa jela Marekani afungwa



Kiarabu ni marufuku katika miskiti Ujerumani



Atumia vidonge vya nguvu za kiume kuzoa kura



Simba apata makao mapya Afrika Kusini



Panya wailazimu Uingereza kukodisha paka



Mtu mrefu duniani awasili Mauritius



Safari ya ndege yakatizwa kutoa salamu za mwisho


TOP 10 YA HAT-TRICKS ZA UEFA CHAMPIONS LEAGUE


Ronaldo-11

Baada ya Ronaldo kupiga hat-trick dhidi ya  Wolfsburg na kuisaidia klabu yake ya Real Madrid kuvuka hatua ya robo fainali na kutinga nusu fainali ya michuano ya klabu bingwa barani Ulaya, mtaani imekuwa ni gumzo kila kona kila ofizi vijiweni na sehemu mblambali hadi maofisini.
Kwa mujibu wa matandao wa sokkaa, hii ndiyo top ten ya hat-trick za kukukumbukwa zaidi kwenye michuano ya Champions League.
10. Mario Gomez vs FC Basel, March 2012
Gomez
Mshambuliaji wa zamani wa Bayern Munich licha ya kuihama klabu hiyo, lakini jina lake litaendelea kukumbukwa kwenye historia ya vitabu vya klabu hiyo.
The Bavarians ilianza kampeni zake kwenye michuano ya klabu bingwa Ulaya mwaka 2012 kwa kupoteza mchezo kwanza wakiwa ugenini kwa bao 1-0 dhidi ya Basel.
Mchezo wa marudiano iliandikwa historia mpya, Robben na Ribbery walikuwa hawakamatiki kwenye mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la Alianz Arena. Nyota wa mchezo huo alikuwa ni Gomez ambaye alikamilisha hat-trick ndani ya dakika 23. Lakini mwisho wa siku miamba hiyo ya Bundesliga iliangukia pua kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Chelsea.
9. Thiery Henry vs Roma, November 2002
Thierry Henry
Msimu wa 2002/2003 klabu bingwa Ulaya, Mfaransa huyo aliibeba Arsenal kwenye mchezo wa ugenini dhidi ya klabu ya AS Roma ya Italia akifanikiwa kupachika bao tatu wavuni timu yake ikitoka na ushindi wa magoli 3-1. Kiwango chake kwenye usiku huo kilikuwa mwiba kwa timu ya Romba mbele ya mashabiki wao wa nyumbani.
8. Kaka vs Anderlecht, November 2006
Kaka
Kiungo mchezeshaji wa kibrazil Kaka atakuwa anakumbukwa kwa mchango wake mkubwa akiwa amevalia uzi wa AC Milan.
Many will remember his demolition of Manchester United at Old Trafford few years ago. One of the greatest moment was against Anderlecht. He bagged his hat-trick in a 4-1 win to give AC Milan hope of progressing to the knock out stage.
Wengi watamkumbuka kwa tukio la kuiangamiza Manchester United kwenye uwanja wa Old Trafford miaka kadhaa iliyopita. Moja ya matukio ya kukumbukwa ni hat-trick yake dhidi ya Anderlecht wakati AC Milan ikishinda kwa bao 4-1na kufufua matumaini ya kusonga mbele kwenye hatua ya mtoano.
7. Wayne Rooney vs Fenerbache, September 2004
Rooney
Nahodha huyu wa Manchester United alicheza mchezo wake wa kwanza wa klabu bingwa Ulaya September 28,  2004 dhidi ya Fenerbache na kufunga hat-trick yake ya kwanza kwenye michuano hiyo mikubwa barani Ulaya ngazi ya vilabu.
Wakati huo Rooney alikuwa na miaka 18 na kumfanya kuwa miongoni mwa wenye umri mdogo zaidi kufunga hat-trick kwenye michuano hiyo.
6. Ronaldinho vs Udinese, September 2005
Ronaldinho
Kwenye wakati wake Ronaldinho hakuwa tu mburudishaji kwenye upande wa soka bali alikuwa mchezaji mwenye uwezo wa kufanya chochote uwanjani. Wakati wowote alikuwa anaweza akamuacha beki kwa chenga za maudhi na kutoa pande la goli au yeye mwenyewe kuzama kambani.
Hat-trick yake dhidi ya Udinese ni moja kati ya nyakati za kukumbukwa zaidi kwenye michuano ya Ulaya.
5. Lionel Messi vs Leverkusen, March 2012
Messi-Leverkusen
Kwa muda mrefu mshambulizi wa Barcelona Lionel Messi amekuwa akitawala mihuano ya Champions League , muargentina huyu anauwezo mkubwa wa kuichambua safu za ulinzi za timu nyingi.
Messi alikuwa mchezaji wa kwanza kufunga magoli matano kwenye mechi moja ya Champions League. Barcelona ilishinda kwa magoli 7-1 kwenye usiku huo na ushindi wa jumla (aggregate) ilikua ni magoli 10-1.
4. Cristiano Ronaldo vs Ajax, October 2012
Ronaldo v ajax
Ukizungumzia maajabu ya Lionel Messin kwenye michuano ya Ulaya huwezi kuacha kutaja uwezo wa mchezaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo. Mshambuliaji huyo wa zamani wa Manchester United alikuwa hazuiliki na akafanikiwa kutumbukia nyavuni mara tatu kwenye mchezo ambao Madrid ilishinda kwa magoli 4-1 dhidi ya mabingwa wa Uholanzi Ajax Amsterdam
3. Ronaldo vs Manchester United, April 2003
Ronaldo el fenomeno
Raia huyu wa Brazil anayefahamika zaidi kwa jina la El Phenomeno alipiga hat-trick dhidi ya Manchester United na kuisaidia timu yake kutinga hatua ya nusu fainali ya Chamipons League mwaka 2003.
Jambo la kukumbukwa zaidi ni pale wakati anatoka uwanjani baada ya kufanyiwa sub dakika ya 65, umati wote wa Old Trafford ulisimama kumshangilia pamoja na mashabiki wa United.
2. Lionel Messi vs Arsenal, April 2010
Messi 2
Mwaka 2010 kwenye mchezo wa robo fainali ya pili, Messi pekeyake alitosha kuiangamiza Arsenal kwa kutandika magoli manne na kuivusha timu yake hadi hatua ya nusu fainali.
  1. Ronaldo vs Wolfsburg, March 2016
Ronaldo
Usiku wa April 12 nyota wa Real Madrid alikuwa hazuiliki. alifunga magoli matatu dhidi ya  Wolfsburg na kuisaidia timu yake kupindua matokeo ya mchezo wa kwanza ya kipigo cha bao 2-0 wakiwa ugenini.

PATA TASWIRA 18 NAMNA BARCELONA ILIVYOVULIWA UBINGWA NA 'MASELA' WA MADRID

ATLETICO MADRID NDIYO WALIOIVUA BARCELONA UBINGWA WA LIGI YA MABINGWA ULAYA. IMEICHAPA MABAO 2-0, CHEKI PICHA NAMNA MAMBO YALIVYOKUWA...



















14 Apr 2016

Related Posts

PICHAZ; KOBE BRAYANT ALIVYOSTAAFU RASMI, JAY Z, DAVID BECKHAM, MASTAA KIBAO WAHUDHURIA



Hakuna refu lisilokuwa na ncha. Mcheza kikapu maarufu wa Marekani, Kobe Bryant amestaafu.

Nyota huyo wa LA Lakers amestaafu na kuagwa na mashabiki kibao wakiwemo nyota wa muziki kama Jay Z, soka wakiongozwa na David Beckham na kikapu wakiongozwa na Magic Johnson.

Katika siku ya kuagwa, Kobe aliyecheza kwenye NBA kwa miaka 20 aliingoza Lakers kushinda kwa pointi 101-96 dhidi ya Utah Jazz huku yeye akifunga pointi 60 na kuweka rekodi ya aina yake.




















14 Apr 2016


Next
JULIO AFUNGUKA, ASEMA YANGA, AZAM WAMEZOEA KUDEKEZWA, HAWATAKI WENGINE WAWE MABINGWA
Previous
MASHABIKI AL AHLY WAONDOKA NA NEMBO YA SIMBA, WATAITUMIA
 
Supported by AMAGA Media services : | |
Copyright © 2015. UKURASA WA HABARI - All Rights Reserved
Templete Designed by Abdallah Magana
Proudly powered by Blogger