MATOKEO,MSIMAMO NA UCHAMBUZI WA LIGI KUU NCHINI ENGLAND WIKIENDI HII

Tables

#   Team MP W D L F A D P Last 5 matches H2H
1 5 5 0 0 15 4 +11 15 W W W W W
2 Previous rank: 4 5 4 1 0 10 3 +7 13 W W W W D
3 Previous rank: 7 5 3 2 0 8 2 +6 11 W W D W D
4 Previous rank: 8 5 3 1 1 12 7 +5 10 W W W D L
5 Previous rank: 2 5 3 1 1 10 6 +4 10 L D W W W
6 Previous rank: 11 5 3 1 1 11 8 +3 10 W W D L W
7 Previous rank: 3 5 3 0 2 8 6 +2 9 L L W W W
8 Previous rank: 17 5 2 1 2 7 5 +2 7 W W D L L
9 Previous rank: 18 5 2 1 2 10 9 +1 7 W W L L D
10 5 2 1 2 6 5 +1 7 W L D L W
11 Previous rank: 9 5 2 1 2 7 7 +0 7 W L W D L
12 Previous rank: 5 5 2 1 2 6 7 -1 7 L D L W W
13 Previous rank: 6 5 1 2 2 5 7 -2 5 L L D W D
14 Previous rank: 15 5 1 2 2 4 6 -2 5 W L D L D
15 Previous rank: 14 5 1 1 3 4 7 -3 4 L D L L W
16 Previous rank: 13 5 1 1 3 3 8 -5 4 L D L W L
17 Previous rank: 19 5 1 1 3 3 9 -6 4 L W D L L
18 Previous rank: 12 5 1 0 4 7 13 -6 3 L L L W L
19 Previous rank: 16 5 0 1 4 3 9 -6 1 L L D L L
20 5 0 1 4 3 14 -11 1 L L L L D
UEFA Champions League
UEFA Champions League Qualifiers
UEFA Europa League
Relegation

MANENO YA JOSE MOURINHO NA WALTER MAZZARRI BAADA YA WATFORD KUSHINDA 3-1 DHIDI YA MAN UNITED

United manager Jose Mourinho looks anxious on the bench as they fall behind during the first period

1Bosi wa Watford Walter Mazzarri: “Ni pointi tatu muhimu zitakazosaidia kuwaongezea wachezaji wangu kujiamini kwenye michezo inayofuata.
“Tumecheza vizuri sana, tuliruhusu goli kwasababu tuliacha kucheza. Tulikuwa na hofu na tulipofanya mabadiliko kila kitu kikawa shwari, ni kitu ambacho tunapaswa kufanyia kazi.
“Kimsingi siangalii sana haya matokeo lakini naangalia namna gani tumecheza. Tumekuwa tukiimarika siku hadi siku kwa kiwango kikubwa.”
Alipoulizwa kama anaweza kukaa meza moja na Mourinho na kupata kinywaji, Mazzarri ambaye wakati yuko Napoli aliwahi kukwaruzana na Mourinho wakati yuko Inter Milan alisema: “Kama ana muda basi sina tatizo tutatekeleza hilo. Kabla ya mechi tulizungumza, hata ikitokea siku yoyote wiki ijayo ikapatikana nafasi basi tutapata wote kwa pamoja chakula cha usiku.”
Bosi wa Manchester United Mourinho: “Nimepata mambo matatu kutoka kwenye mchezo huu, lakini moja tu kati ya hayo yote naweza kurekebisha.
“Sababu ya kwanza kutokana na makosa yetu wenyewe, inahusisha makosa ya mtu mmoja mmoja na ya kitimu kwa maana ya mchezaji mmoja-mmoja na timu kwa ujumla. Lazima tuhakikishe tunafanya marekebisho ili kuimarika, suala hilo liko mikononi mwetu.
“Sababu ya pili ni mwamuzi na siwezi kuvumilia kunyamazia makosa yao.
“Sababu ya tatu ni bahati, hatukuwa na bahati. Wakati tunafungwa mchezo huu sisi ndio tulikuwa timu bora.”

Comments

Diamond Platnumz ft Rayvanny Salome ( Traditional Official Music video)

 


Wakali kutokea kiwanda cha Bongofleva Naseeb Abdul a.k.a Diamond Platnumz pamoja na Raymond a.k.a Rayvanny wakitokea katika Laber ya WCB leo September 18 2016 wanayofuraha kushare na sisi mdundo wao mpya unaoitwa ‘Salome‘ 
Tayari nimekusogezea hapa chini video yao, ukimaliza kuitazama niachie comment yako kuniambia wametisha kwa asilimia ngapi.

MAN UNITED YANYUKWA EPL


WATFORD-MANUNITED                                                                                                                                                     WAKICHEZA Ugenini huko Vicarage Road Manchester United Leo wamefungwa Bao 3-1 na Watford kwenye Mechi ya EPL, Ligi Kuu England.
Hii ni mara ya kwanza kwa Watford kuifunga Man United katika Miaka 30.
Bao za Watford zilufungwa Dakika za 34, 83 na Penati ya Dakika ya 94 kupitia Etiene Capoye, Juan Zaniga na Troy Deeney.
Bao la Man United lilufungwa na Marcus Rashford katika Dakika ya 62.
Kwenye EPL hiki ni kipigo cha pili mfululizo kwa Man United baada ya Wikiendi iliyopita kufungwa pia na Man City lakini pia Juzi kati Wiki walichapwa 1-0 huko Rotterdam na Feyenoord kwenye Mechi yao ya kwanza ya Kundi lao la UEFA EUROPA LIGI.
Mechi inayofuata kwa Man United ni Jumatano Ugenini na Northampton ikiwa ni Mechi ya Raundi ya 3 ya EFL CUP ambalo ni Kombe la Ligi.
VIKOSI VILIVYOANZA:
Watford (3-5-2) Gomes; Cathcart, Prödl, Britos; Janmaat, Pereyra, Behrami, Capoue, Holebas; Deeney, Ighalo.
Akiba: Pantilimon, Zuniga, Kenedy, Watson, Amrabat, Guedioura, Success.
Manchester United (4-2-3-1) De Gea; Valencia, Bailly, Smalling, Shaw; Fellaini, Pogba; Rashford, Rooney, Martial; Ibrahimovic.
Akiba: Romero, Blind, Carrick, Herrera, Mata, Young, Memphis.
REFA: Michael Oliver

Chadema yalia na majipu na ubaguzi


Benard Mwakyembe, Kaimu Mwenyekiti wa Dar es Salaam kubwa(Great Dar es Salaam)ya Chadema
Benard Mwakyembe, Kaimu Mwenyekiti wa Dar es Salaam kubwa(Great Dar es Salaam)ya Chadema
CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimemtaka Rais John Magufuli kutumbua majipu makubwa yaliyokuwepo ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kufuata taratibu za uongozi kwenye utumbuaji huo
Benard Mwakyembe, Kaimu Mwenyekiti wa Dar es Salaam kubwa(Great Dar es Salaam)ya Chadema amesema kuwa utumbuaji wa majipu mbele ya umma ni kinyume na taratibu za uongozi akitaja mfano wa kusimamishwa kazi hazalani kwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Wilson Kabwe sio utaratibu nzuri kwani angiitwa na kuchuunguzwa
“Ingawa ni vema kuwawajibisha viongozi wazembe lakini Rais anafanya maamuzi kwa mzuka wa ushabiki wa watu pasi nakufuta taratibu za uongozi”amesema Mwakyembe.
Mwakyembe amesema kuwa nyuma ya pazia la utumbuaji majipu kuna majipu makubwa ambapo utaratibu wa kuhojiwa kwa waliotumbuliwa utafanya kupatikana kwa mizizi ya majipu hayo.
“Nyuma ya Wilson Kabwe kuna Mstahiki Meya aliyemaliza Muda wake ambaye ni Didas Masaburi naye alipaswa kuwajibishwa kama mtuhumiwa kutokana na kuwa yeye ni mtu wa pili kusaini mikataba yote ya Jiji .
Na madiwani wote aliohusika na viongizi wote wa serikali wawajibishwe” amesema Mwakyembe.
Aidha alisema kuwa wamesikitishwa na kitendo cha Magufuli kutumia kumbagua Meya wa Jiji la katika ufunguzi wa daraja la Julius Nyerere maarufu kama daraja la Kigamboni baada ya kumfanya awe kama mvamizi kwenye uzinduzi huo.
Henri Kileo Katibu Mkuu Dar es Salaam Kubwa amesma kuwa Mkuu wa Mkoa ni kinara wa vitendo vya ubaguzi wa viongozi wa upinzani ili kuwadhoofisha .
Kadhia hiyo ya ubaguzi imehusishwa pia kwa Shirika la Taifa la Utangazaji (TBC) kutorusha matangazo au habari inayowahusu wapinzani.
Katibu Mkuu wa Great Dar es Salaam, alisema siku ya uzinduzi wa daraja hilo Mstahiki Meya alipokuwa anahutubia baada ya kupewa nafasi TBC walizima matangazo.
Mwakyembe anasema kuwa kwa shirika hilo kutorusha matangazo ya vyama vya upinzani sio mara ya kwanza kwani wao  hawarushi matangazo ya aina yoyote yale yanayowalenga wapinzani
“ikiwa ile ni chombo cha habari cha taifa kinochoendeshwa kwa kodi za wananchi  lakini wanahubiri ubaguzi ikiwa na vyama navyo ni vya walipa kodi vilivyosajiliwa kwa mujibu wa katiba.
Kama wanataka iwe hivyo basi waifanye TBC iwe kama Radio Uhuru ya CCM wananchi wajue kwamba ni shirika la  utangazaji la CCM” amesema Mwakyembe.

Chanzo;Mwanahalisionline

NMB yazindua Business Club Ifakara

 
NMB
Mkuu wa Wilaya ya Kilombelo Mhe. Leph Benjamini Gembe akifungua pazia kuashiria uzinduzi rasmi wa NMB Business Club ndani ya Mji wa Ifakara. NMB Business Club inawakusanya wafanyabiashara wote wanaowezeshwa na NMB kwa lengo la kuwaendeleza kibiashara. Business Club hii itakuwa ya 33 kuzinduliwa katika mikoa tofauti nchini kusudi likiwa kuwaunganisha wafanyabiashara wote nchini waweze kufaidika na huduma za NMB, Meneja wa NMB Kanda ya Mashariki, Bw. Nazareti Lebbi akishuhudia uzinduzi huo.
????????????????????????????????????
Mkuu wa Wilaya ya Kilombelo Mhe. Leph Benjamini Gembe akifurahia uzinduzi rasmi wa NMB Business Club ndani ya Mji wa Ifakara. NMB Business Club inawakusanya wafanyabiashara wote wanaowezeshwa na NMB kwa lengo la kuwaendeleza kibiashara. Business Club hii itakuwa ya 33 kuzinduliwa katika mikoa tofauti nchini kusudi likiwa kuwaunganisha wafanyabiashara wote nchini waweze kufaidika na huduma za NMB, kwanza kulia ni Meneja wa NMB Kanda ya Mashariki, Bw. Nazareti Lebb na kushoto ni Meneja wa NMB tawi la Ifakara Bw. William Kaitira.
NMB imeendelea kuwa kinara katika kubuni na kuboresha huduma mbali mbali za kibenki, ili kuwawezesha wateja wake kupata unafuu na urahisi wa upatikanaji wa huduma za kibenki nchini Tanzania. NMB pia inatambua mahitaji ya wateja yanatofautiana, hivyo basi uzinduzi wa NMB Business Clubs una lengo la kuwafikia wafanyabiashara wadogo, wa kati na wakubwa walioko Ifakara na Wilaya ya Kilombero kwa Ujumla. Wafanyabiashara hawa ni sehemu ya wafanyabiashara zaidi ya 50,000 ambao ni wateja wa NMB nchi nzima.
Hii ni Business Club ya 33 kuzinduliwa na NMB ambapo nyingine ziko katika mikoa tofauti nchi nzima, na kuna mpango wa kuongeza moja zaidi kabla ya mwisho wa maka. Dhumuni kubwa ni kuwaunganisha wafanyabiashara wote nchini waweze kufaidika na huduma za NMB ambazo pia zitawawezeshakujikimu kimaisha. Hadi sasa NMB Business Clubs zina zaidi ya wafanyabiashara 10,000 waliojiunga.

Madhehebu ya shia yaunga mkono kasi ya Rais Magufuli

 
kigogo1Shekh Hemed Jalala akifafanua jambo kwa wanahabari
KASI  ya Rais, Dkt. John Pombe Magufuli inazidi kushika moto baada ya Kiongozi Mkuu wa Chuo cha Kiislam (Hawza) Imam Swadiq ambaye pia ni Kiongozi Mkuu wa Waislam wa Madhehebu ya Shia Ithnasheria, Tanzania,  Shekh Hemed Jalala amewataka Watanzania na waumini wa madhehebu yote nchini kumuunga mkono kwa kasi yake.
Shehe Jalala akizungumza leo na wanahabari katika maadhimisho ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mmoja wa  wanafunzi wa Mtume Mohamed (S.A.W),  Imam Ali (A.S), amesema alikuwa kiongozi jasiri, mpenda haki,  aliyepinga rushwa, muwajibikaji na mpinga ufisadi, kama ilivyo kwa sasa kwa Rais Magufuli ambaye ameonesha nia ya dhati ya kuifanya Tanzania kuwa mpya kwa kupinga ufisadi, rushwa  na mambo mengine ambayo yanawaumiza Watanzania wa hali ya chini.
“Tunaadhimisha zaidi ya miaka  1430 ya kuzaliwa kwake
Imam Ali kwa kuwa alikuwa mwanafunzi bora wa kuigwa kwa kile alichokipigania ndicho kinachoonekana kwa Rais Magufuli, viongozi wa dini tuwaongoze waumini wetu katika kumuombea na kukemea pale tunapoona si sahihi, ila mpaka hapa tulipo ameonesha dira ya Tanzania mpya,” alisema Shehe Jalala.
Na Mwandishi Wetu/ GPL
 
Supported by AMAGA Media services : | |
Copyright © 2015. UKURASA WA HABARI - All Rights Reserved
Templete Designed by Abdallah Magana
Proudly powered by Blogger