Magazeti ya Tanzania yalichoandika leo April 5 2016

CUF Yatangaza Rasmi kutomtambua Rais Dkt. Shein na Serikali yake.....Tamko lao Liko Hapa

MAAZIMIO YA BARAZA KUU LA UONGOZI LA TAIFA LA CHAMA KATIKA KIKAO CHAKE CHA TAREHE 2 – 3 APRILI, 2016 KILICHOFANYIKA MAZSONS HOTEL, MJINI ZANZIBAR
Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la THE CIVIC UNITED FRONT (CUF – Chama Cha Wananchi) limefanya kikao chake cha kawaida kwa siku mbili, tarehe 2 hadi 3 Aprili, 2016 mjini Zanzibar chini ya Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Chama, Mheshimiwa Twaha Taslima.
Ajenda kuu ya kikao hicho ilikuwa ni Hali ya Kisiasa Zanzibar na mwelekeo wa CUF baada ya kufanyika kile kilichoitwa uchaguzi wa marudio wa tarehe 20 Machi, 2016.
Baada ya kupokea na kujadili kwa kina ajenda hiyo, Baraza Kuu la Uongozi la Taifa limefikia maazimio yafuatayo:
1. Linawapongeza wananchi wote wa Zanzibar kwa ujasiri, uzalendo na ari kubwa walioionesha kwa kuitikia kwa kiasi kikubwa wito wa chama chao cha CUF wa kuwataka wasishiriki katika uhuni na ubakaji wa demokrasia uliopewa jina la uchaguzi wa marudio wa tarehe 20 Machi, 2016.
Baraza Kuu la Uongozi limefurahishwa kuona zaidi ya asilimia 80 ya wapiga kura wa Zanzibar hawakujitokeza kushiriki katika uchaguzi huo haramu na batili, na hivyo kuudhihirishia ulimwengu kwamba Chama Cha Mapinduzi (CCM) hakina ridhaa ya wapiga kura hao.
2. Linawapongeza waliokuwa wagombea wa CUF kwa nafasi zote za Urais, Uwakilishi na Udiwani kwa kuheshimu maamuzi ya Chama na kutoshiriki uchaguzi haramu na batili wa marudio licha ya njama nyingi zilizokuwa zikifanywa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar chini ya Mwenyekiti wake, Jecha Salim Jecha, za kulazimisha ushiriki wao. Msimamo wa wagombea hao umewadhihirishia na kuwathibitishia CCM kwamba tofauti na wao, viongozi wa CUF hawajali nafasi na vyeo binafsi bali wanachotaka ni kuleta mabadiliko ya kweli kwa maslahi ya watu wote wa Zanzibar.
3. Linawapongeza kwa namna ya pekee wagombea Urais, Uwakilishi na Udiwani wa vyama vyengine vya upinzani ambavyo ni UMD, JAHAZI ASILIA, CHAUMMA, UPDP, DP, na ACT-WAZALENDO, na vile vinavyoshirikiana kupitia UKAWA ambavyo ni CHADEMA, NCCR na NLD vilivyoungana na wananchi wa Zanzibar kususia uchaguzi haramu na batili wa marudio na kusimamia maamuzi halali ya wapiga kura waliyoyafanya kupitia uchaguzi mkuu halali wa tarehe 25 Oktoba, 2015.
4. Linazishukuru na kuzipongeza jumuiya na taasisi zote za kitaifa na kimataifa pamoja na nchi rafiki za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambazo zilikataa kuleta waangalizi wa uchaguzi katika uchaguzi huo haramu na batili na hivyo kuungana na Wazanzibari katika kutetea maamuzi yao halali waliyoyafanya katika uchaguzi mkuu halali uliokuwa huru na wa haki wa tarehe 25 Oktoba, 2015.
5. Linavishukuru na kuvipongeza vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi pamoja na waandishi wa habari na wapiga picha kwa jinsi vilivyosaidia kuonesha ulimwengu uchaguzi mkuu uliokuwa halali, huru na wa haki wa tarehe 25 Oktoba, 2015 na pia kwa jinsi vilivyoanika uchafuzi wa tarehe 20 Machi, 2016 hasa kule kuonesha vituo vya kupigia kura vikiwa havina watu na hivyo kuwasaidia Watanzania na ulimwengu kuujua ukweli ambao CCM na Tume yao ya Uchaguzi walikuwa wakijaribu kuuficha.
6. Linalaani tabia na mwenendo wa uongo, uzushi, na uvunjwaji wa Katiba, Sheria na Maadili wa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, Jecha Salim Jecha, dhidi ya matakwa na maamuzi halali ya Wazanzibari waliyoyafanya katika uchaguzi mkuu huru na wa haki wa tarehe 25 Oktoba, 2015 na kitendo chake cha kuiingiza Zanzibar katika dimbwi la chuki, uhasama, uvunjifu wa haki za binadamu na udhalilishaji wa raia kwa sababu tu ya kukiridhisha chama chake cha CCM ambacho kimekataliwa na Wazanzibari.
Vitendo vya Jecha Salim Jecha vimeishushia hadhi Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar na kuichafulia jina Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mbele ya jumuiya ya kimataifa na kuonekana haiko tofauti na nchi nyengine za Afrika zisizoheshimu matakwa na maamuzi ya wananchi katika uchaguzi.
7. Linalaani hatua ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. John Pombe Magufuli kuleta nguvu kubwa ya vikosi vya ulinzi na usalama kuja kubaka demokrasia Zanzibar. 
Baraza Kuu linalaani vikali nguvu kubwa iliyotumiwa na vyombo vya dola dhidi ya raia wasio na hatia kwa lengo na madhumuni ya kuwatisha na kuwazuia wasitumie haki zao za msingi kama ibada kwa kuwalazimisha kutotoka nje ya nyumba zao kuanzia saa 2 usiku wakati muda huo ni muda wa ibada ya sala kwa Waislamu ambao ni asilimia 99 ya wananchi wote wa Zanzibar. 
Baraza Kuu pia linalaani mwenendo wa viongozi wa juu wa vyombo vya ulinzi na usalama wa kutumika waziwazi kisiasa kwa kuegemea upande wa CCM na kuwakandimiza viongozi na wanachama wa CUF kinyume na maadili ya kazi zao.
8. Linalaani vitendo vya Serikali kuunda makundi ya kiharamia ambayo yamekuwa yakiwahujumu raia wasio na hatia yakitumia silaha za moto na silaha za kienyeji huku yakitumia gari za Idara Maalum za SMZ. 
Baraza Kuu linalaani Jeshi la Polisi ambalo limekuwa likiyalinda makundi haya na kutochukua hatua zozote dhidi yao licha ya wananchi wanaohujumiwa kutoa taarifa kwa jeshi hilo. 
Badala yake, katika matukio mengi Polisi imewageuzia kibao wananchi waliohujumiwa kwa kuwakamata na kuwaweka ndani. 
Baraza Kuu linawataka Wakuu wa Jeshi la Polisi kujirudi, kutekeleza majukumu yao ya kulinda usalama wa raia na mali zao na na kufuata maadili yao na kuwacha kujifanya ni Idara ya Polisi ya CCM.
9. Haliyatambui matokeo ya uchaguzi huo haramu na batili, na kwa msingi huo halimtambui Dk. Ali Mohamed Shein kuwa Rais wa Zanzibar, haliwatambui waliotangazwa kuwa Wawakilishi na wala haliwatambui waliotangazwa kuwa Madiwani.
Baraza Kuu linaungana na wananchi wa Zanzibar waliokataa kuwapa uhalali watu hao na kwa hivyo halitoitambua Serikali, Manispaa na Halmashauri za Wilaya zitakazoundwa na watu hao. 
CUF haitoshirikiana na Serikali itakayoundwa kwa sababu ni kinyume na Katiba ya Zanzibar, kinyume na Sheria ya Uchaguzi na haikutokana na ridhaa ya watu. 
Kwa vyovyote vile, Serikali itakayoundwa haitakidhi matakwa ya Katiba ya Zanzibar na hivyo CUF haitoshiriki kwenye uvunjaji wa Katiba ambayo inaeleza kwa uwazi kabisa namna ya kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar.
10. Linawataka wananchi wote wa Zanzibar kutumia njia za amani, za kikatiba na kisheria ambazo zimewahi kutumika katika nchi nyingine duniani kuwakataa watawala waovu na wasio na ridhaa ya watu waliojiweka madarakani kwa kutumia nguvu na ubakaji wa demokrasia kwa kutoipa ushirikiano Serikali itakayoundwa na watawala hao.
11. Linaendelea kuutambua uchaguzi mkuu uliokuwa halali, huru, wa haki na uliofanyika katika hali ya amani na utulivu wa tarehe 25 Oktoba, 2015 na pia linayatambua matokeo yake ambayo yalionesha wazi kwamba chaguo la Wazanzibari ni CUF na Maalim Seif Sharif Hamad kuiongoza Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar. 
Kitendo cha zaidi ya asilimia 80 ya Wazanzibari kususia uchaguzi haramu na batili wa tarehe 20 Machi, 2016 kimezidi kuyapa nguvu maamuzi yao ya tarehe 25 Oktoba, 2015 mbele ya macho ya Watanzania na dunia.
12. Linaendelea kuwataka Wazanzibari kuwa watulivu na kulinda amani iliyopo na linawahakikishia kwamba CUF inaendelea na juhudi zake za kutafuta haki yao na kusimamia maamuzi yao waliyoyafanya tarehe 25 Oktoba, 2015 kwa njia za amani na za kidemokrasia. Njia hizo za amani zimefanikiwa na kuungwa mkono na jumuiya ya kimataifa ambayo imeanza kuchukua hatua dhidi ya ubakwaji wa demokrasia uliofanyika.
13. Linazishukuru na kuzipongeza nchi washirika wa maendeleo kwa kuchukua maamuzi ya kuzifutia misaada Serikali za kidikteta za CCM ambazo zimebaka demokrasia na kukanyaga haki za wananchi wa Zanzibar.
Baraza Kuu linatoa wito kwa nchi hizo washirika wa maendeleo na jumuiya za kimataifa kuchukua hatua zaidi dhidi ya Serikali za CCM na madikteta wake walioshiriki katika ubakaji wa demokrasia Zanzibar zikiwemo hatua makhsusi dhidi ya watu makhsusi waliohusika na ubakaji huo wa demokrasia na uvunjaji wa haki za binadamu katika kipindi hiki.
MWISHO, Baraza Kuu la Uongozi la Taifa linawahakikishia wanachama wake wote na Watanzania kwa ujumla kwamba chama chao kiko imara na hakitoyumba wala kuyumbishwa katika kutetea na kupigania haki zao hadi tutakapofanikisha ujenzi wa taifa imara linalosimamia na kuheshimu utawala wa sheria, haki za binadamu, demokrasia na utu wa watu wote.

BREAKING: Unakumbuka alichokifanya Rais Magufuli sherehe za Uhuru? leo katangaza kingine

  Miongoni mwa vitu vikubwa vilivyomuweka kwenye headlines Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli toka aingie madarakani ni pamoja na kutangaza kusitisha shamrashamra za sherehe za uhuru na shilingi bilioni nne iliyokua itumike kwenye sherehe hizo kitaifa ikapelekwa kwenda kutengeza barabara.
Sasa leo habari mpya ni kwamba Rais Magufuli ameahirisha shamrashamra za maadhimisho ya siku ya Muungano kwa mwaka huu ambayo huadhimishwa kila tarehe 26 ya Mwezi Aprili na badala yake ameelekeza kuwa siku hiyo itakuwa ya mapumziko kama kawaida na watanzania waiadhimishe wakiwa majumbani kwao ama katika shughuli zao binafsi.
Kufuatia kuahirishwa kwa shamrashamra hizo, Rais Magufuli ameelekeza kuwa fedha zilizopangwa kutumika kwa ajili ya kugharamia vinywaji, vyakula, gwaride, halaiki, burudani mbalimbali na hafla ya usiku ambazo ni zaidi ya shilingi Bilioni 2, zitumike kuanzisha upanuzi wa barabara ya “Mwanza – Airport” katika eneo linaloanzia Ghana Quaters hadi Uwanja wa Ndege wa Mwanza.
Barabara hiyo inafanyiwa upanuzi ili kukabiliana na kero ya msongamano mkubwa wa magari ambao unaathiri shughuli za kila siku za wananchi.

Utatamani kujua maamuzi yaliyotangazwa leo Mahakamani kwenye ile kesi ya Mrema na Mbatia

Nani mbunge halali wa Vunjo? kumbuka baada ya uchaguzi mkuu mwaka 2015 James Mbatia alitangazwa mshindi wa jimbo la Vunjo ambalo lilikua chini ya Mrema kipindi kilichopita, baada ya huo ushindi Mrema alifungua kesi Mahakamani baada ya kudai amechezewa mchezo mchafu na yeye ndio alistahili kuwa mshindi.
Kesi ikaendelea mpaka leo April 4 2016 maamuzi mapya kutangazwa kwamba Mahakama kuu kanda  ya Moshi imeridhia makubaliano yaliyofikiwa kati ya Mbunge wa Vunjo James Mbatia na Agustino Mrema hivyo Mahakama chini ya jaji  Lugano Mwandambo imeridhia shauri hilo kuisha na kwamba James Mbatia ndiye Mbunge halali wa Vunjo na Mrema atatakiwa kulipa sehemu ya gharama za mawakili wa Mbatia shilingi Milioni 40.
Mbatia 2
Mrema hakuonekana Mahakamani leo na aliwakilishwa na Wakili wake January Nkobogo ambapo James Mbatia aliyehudhuria Mahakamani leo alisema yafuatayo >>> ‘siku ya leo tumeandika historia mpya hasa kwa jimbo letu la Vunjo, kwa kuwa ukweli ni msingi wa haki na Wanasheria wetu sita waliokua wananitetea mimi
Baada ya mlalamikaji Mzee wetu Mrema kufikia hatua ya kutoa ushahidi Mahakamani baada ya ushahidi alioutoa Mahakamani  na maswali aliyoulizwa yeye mtu mzima akaona upepo sio mzuri kwa upande wake, alipoliona hilo kiutu uzima baada ya kushauriwa na kuona jasho lililomtoka Mahakamani wiki iliyopita akaona hali inazidi kuwa mbaya upande wake
Mbatia 3
James Mbatia kwenye sentensi nyingine amesema >>> ‘Ndugu Mrema amekubali au kukanusha yale yote aliyoleta Mahakamani na ushahidi wake wote aliosema Mahakamani na malalamiko dhidi yangu, Wanavunjo, dhidi ya taasisi za kidini yooote ameyakanusha kwenye hati ya makubaliano, hilo ndio lilikua la msingi ameyakanusha na amesaini mwenyewe’
IMG-20160404-WA0043
La pili, Mrema amekubali kuwa James Mbatia ndio mbunge halali aliyechaguliwa jimbo la Vunjo, swala la tatu alilokubali ni kweli tungeweza kumdai gharama kubwa, mimi binafsi nimeingia gharama kubwa ikiwemo ya usafiri toka November 2015 alivyoleta shauri hili Mahakamani, sijamdai gharama kwa upande wangu hata senti moja, nimemsamehe kama kawaida yangu‘ – James Mbatia
Cha kumalizia Mbatia amesema ‘Kuna gharama kubwa ambazo ziliingia upande wa jopo lote la Mawakili na amekubali yeye mimi nilipe asilimia 50 ya gharama za mawakili na yeye alipe 50, kwahiyo Mrema amekubali kulipa Mawakili sehemu tu ya gharama ya MILIONI 40 kwa Mawakili wetu na ni agizo la Mahakama na imeingia Mahakamani, kwa hatua ya kwanza MILIONI 15 Mawakili wetu watazipata kwa sababu zipo Mahakamani tayari aliziweka deposit, May atalipa nyingine 15 na kabla ya June atalipa 10 zilizobaki na asipofanya hivyo ni kifungo’

CHEKI PICHAAAAZ, BAO LA MARTIAL LILIVYOIPA USHINDI MAN UNITED KWA BAO 1-0 VS EVERTON




Manchester United (4-2-3-1): De Gea 7; Darmian 6.5, Smalling 6, Blind 8 (Valencia 82, 6), Rojo 4 (Fosu-Mensah 45, 7); Carrick 6 (Herrera 58, 6), Schneiderlin 5.5; Mata 6, Lingard 6, Martial 7.5; Rashford 7.
Subs not used: Romero, Young, Depay, Fellaini.
Booked: Smalling, Lingard.
Goal: Martial 54.
Everton (4-3-3): Robles 7; Coleman 6, Stones 7, Jagielka 7, Baines 6; McCarthy 6, Barkley 6 (Niasse 87, 6), Cleverley 6; Deulofeu 7 (Mirallas 63, 6), Lukaku 6, Lennon 6.
Subs not used: Howard, Oviedo, Funes Mori, Besic, Kone.
Referee: Andre Marriner 7.

Star man: Daley Blind. 












MBEYA CITY&BIN SLUM,KUSAINI MKATABA MPYA



SIKU MBEYA CITY ILIPOINGIA MKATABA NA BIN SLUM, HAPA ILIWAKILISHWA NA MMOJA WA WAKURUGENZI WAKE, MOHAMMED BIN SLUM (KULIA).

Mdhamini wa Mbeya City, Nassor Bin Slum amesema anatarajia kuongeza mkataba mwingine wa miaka miwili ya kuidhamini timu hiyo iwapo itabakia ligi kuu msimu ujao.
Mbeya City, ambayo ilikuja kwa kasi wakati ilipopanda ligi kuu msimu wa 2013/14 na kumaliza ikiwa nafasi ya tatu ya msimamo wa iliingia udhamini na Bin Slum kwa muda wa miaka miwili ambao unatarajia kufikia tamati mwishoni mwa msimu huu.
NASSOR BIN SLUM
Hata hivyo, timu hiyo ipo nafasi ya 12 ya msimamo kwa sasa ikiwa na pointi 24 nyuma ya Kagera Sugar yenye pointi 25 na iwapo itafanya vibaya katika mechi zake zilizobakia itakuwa kwenye hatari ya kushuka daraja.
 Bin Slum amesema kuwa, timu hiyo haifanyi vizuri lakini ameridhika na jinsi inavyomtangaza ikiwa ni pamoja na kuheshimu mkataba walioingia na kudai kuwa ataongeza mkataba mwingine wa miaka miwili iwapo timu hiyo itabaki ligi kuu msimu ujao na ikishuka ndiyo anaagana nayo.
“Timu haifanyi vizuri, lakini naridhika na kwa jinsi wanavyonitangaza vyema katika kila mechi wanayocheza, ni watu wanaoheshimu mkataba, Mbeya City wanajitahidi, nitaongeza mkataba mwingine nikimaliza huu na nimewapa masharti, wamesema watajipanga ili kurudisha makali yao ya msimu uliopita.
“Kasi waliyoionyesha msimu huu ni tofauti na msimu uliopita, lakini kwa sasa nipo katika mazungumzo ya kuongeza mkataba mwingine wa miaka miwili ijayo.


“Mkataba wa safari hii nitakaoingia nao utakuwa ni wa masharti tofauti na ilivyokuwa hapo nyuma na iwapo watashuka daraja basi itakuwa ndio mwisho umefikia kwani moja ya masharti yangu ni kudhamini timu ambazo zipo ligi kuu tu,” alisema Bin Slum.
Credit:Salehe jembe

ULIISIKIA HII YA SIMBA KUSHINDA 11-1?




Kikosi cha Simba jana Jumapili kimeendeleza moto wake wa kufanya vizuri katika mechi zake baada ya kuitandika Nidham FC inayomilikwa na Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) mabao 11-1.
Simba inayofundishwa na Mganda, Jackson Mayanja, ilipambana na Nidhamu FC katika mechi ya kirafiki iliyopigwa kwenye Uwanja wa Chuo cha Polisi jijini Dar es Salaam.
Mchezo huo ulikuwa maalum kwa Simba ambayo hivi sasa ipo katika maandalizi makali ya kujiandaa na mechi ya Kombe la FA dhidi ya Coasta Union ya Tanga itakaopigwa Aprili 11, kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, lakini pia michuano ya Ligi Kuu Bara.
Mabao ya Simba katika mechi hiyo yalifungwa na Said Ndemla aliyetupia mawili, Awadhi Juma (2), Daniel Lyanga (2), Ibrahim Ajib (2) pamoja na Musa Hassan ‘Mgosi’ (2) huku lingine likifungwa na kinda wa kikosi B cha timu hiyo.
Kocha Mkuu wa Simba, Jackson Mayanja ameliambia Championi Jumatatu kuwa, pamoja na kikosi chake hicho kupata matokeo hayo bado kinatakiwa kiwe bora zaidi ya hapo.
credit;Salehe Jembe

RATIBA YA UEFA CHAMPIONS LIGI HATUA YA ROBO FAINALI


ROBO FAINALI
**Mechi zote kuanza Saa 3 Dakika 45 Usiku
Jumanne Aprili 5
Bayern Munich v Benfica
Barcelona v Atletico Madrid 

 
**Mechi zote kuanza Saa 3 Dakika 45 Usiku
Jumatano Aprili 6
Paris St-Germain v Manchester City
Wolfsburg v Real Madrid
Marudiano
Jumanne Aprili 12
Manchester City v Paris St-Germain
Real Madrid v Wolfsburg
Jumatano Aprili 13
Benfica v Bayern Munich
Atletico Madrid v Barcelona
UEFA CHAMPIONZ LIGI
TAREHE MUHIMU:
-Droo ya Nusu Fainali: Aprili 15
**Mechi Aprili 26/27 na Marudiano Mei 3/4
FAINALI
Mei 28
San Siro, Milan, Italy

UEFA CHAMPIONS LIGI:BARCA KUTELEZA TENA KAMA EL CLASICO?

 


UEFA CHAMPIONZ LIGI
ROBO FAINALI
**Mechi zote kuanza Saa 3 Dakika 45 Usiku
Jumanne Aprili 5
Bayern Munich v Benfica
Barcelona v Atletico Madrid
++++++++++++++++++++++++++++++
BARCA-HUZUNIJUMANNE Usiku Mabingwa Watetezi wa UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI, FC Barcelona wako kwao Nou Camp Jijini Barcelona Nchini Spain kucheza na wenzao wa Spain Atletico Madrid kwenye Mechi ya kwanza ya Robo Fainali
Mechi nyingine ya Robo Fainali Siku hiyo hiyo ni huko Munich, Germany wakati Bayern Munich watacheza na Benfica ya Portugal.
Barcelona wanaingia kwenye Mechi hii na Atletico Madrid wakitoka kwenye kipigo kitakatifu cha Jumamosi Uwanjani kwao Nou Camp mikononi mwa Mahasimu wao wakubwa Real Madrid waliowachapa 2-1 kwenye Mechi ya La Liga.
Kipigo hicho kilukuwa cha kwanza kwa Barca katika Mechi 39 chini ya Kocha Mkuu wao Luis Enrique.
Mbali ya hilo, Barca wanatinga kwenye Robo Fainali hii wakiwania kuwa Timu ya kwanza tangu Miaka ya 1990 kuweza kutetea vyema Taji lao la Ulaya ambalo wao walishindwa kufanya hivyo Mwaka 2010 na 2012.
Lakini Wachambuzi wengi, hasa wa huko Spain, wamekuwa na wasiwasi na Barca kwa sasa baada ya kuonekana wakiwa goigoi walipofungwa Juzi na Real.
++++++++++++++++++++++++++++++
PATA DONDOO FUPI ZA MECHI HIZO:
Jumanne Aprili 5
BARCELONA v ATLÉTICO MADRID
-Barcelona wameshinda Mechi 6 zilizopita dhidi ya Atletico Madrid lakini katika Mechi yao pekee ya Ulaya, Atletico iliibwaga Barca kwa Jumla ya Bao 2-1 katika Mechi 2 za Robo Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI ya Msimu wa 2013/14.
++++++++++++++++++++++++++++++
Lakini, Kocha Luis Enrique, mara baada ya kipigo toka kwa Real, amesema: “Tushaisahau Gemu hiyo!”
Ingawa Atletico hawana rekodi nzuri dhidi ya Barca, Timu hiyo ya Jiji la Madrid ni wapinzani wagumu na hasa kwa Mechi za Ulaya na Barca watakumbuka vyema nini walitendewa Msimu wa 2013/14 kwenye UCL.
Kwenye Hatua ya Robo Fainali ya UCL, kama hii, Barca walitoka 1-1 na Atletico Uwanjani Nou Camp na kunyukwa 1-0 huko Vicente Calderon na kutupwa nje ya UEAF CHAMPIONZ LIGI.
Hali za Timu
Majeruhi wa Barca ni Mathieu na Adriano na hivyo Luis Enrique ana uwezo wa kushusha Kikosi thabiti.
Kwa upande wa Atletico Madrid, chini ya Kocha Diego Simeone, watafurahia kuwa nae nguzo yao kuu Diego Godin ingawa watamkosa Gimenez ambae pengo lake linaweza kuzibwa na Stefan Savic.
Baada ya Mechi hizi za Jumanne, Jumatano pia zipo Mechi 2 za Robo Fainali za UCL ambapo Paris St-Germain wapo kwao Jijini Paris Nchini France kucheza na Manchester City ya England na nyingine ni huko Germany kati ya Wolfsburg na Real Madrid.
Marudiano ya Robo Fainali hizi ni Aprili 12 na 13.
VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:
Barcelona: Ter Stegen; Alves, Mascherano, Pique, Alba; Rakitic, Busquets, Iniesta; Messi, Suarez, Neymar
Atletico Madrid: Oblak; Juanfran, Godin, Savic, Luis; Koke, Gabi, Tiago, Saul; Griezman, Torres
REFA: Felix Brych  (German)
UEFA CHAMPIONZ LIGI
ROBO FAINALI
**Mechi zote kuanza Saa 3 Dakika 45 Usiku
Jumatano Aprili 6
Paris St-Germain v Manchester City
Wolfsburg v Real Madrid
Marudiano
Jumanne Aprili 12
Manchester City v Paris St-Germain
Real Madrid v Wolfsburg
Jumatano Aprili 13
Benfica v Bayern Munich
Atletico Madrid v Barcelona
UEFA CHAMPIONZ LIGI
TAREHE MUHIMU:
-Droo ya Nusu Fainali: Aprili 15
**Mechi Aprili 26/27 na Marudiano Mei 3/4
FAINALI
Mei 28
San Siro, Milan, Italy

ANTONIO CONTE MENEJA MPYA CHELSEA


CONTE                                                                                                                                                         Chelsea imeteua Bosi wa Timu ya Taifa ya Italy Antonio Conte kuwa Meneja wao mpya.
Conte, mwenye Miaka 46 na aliewahi kuwa Kocha Mkuu wa Juventus, ataanza kazi na Chelsea kwa Mkataba wa Miaka Mitatu baada ya Fainali za EURO 2016 kumalizika.
Kwenye EURO 2016, Kombe la Mataifa ya Ulaya ambalo litachezwa huko France na kwisha Julai 10, Conte ataiongoza Timu ya Taifa.
Akiongelee uteuzi wake huo, Conte amesema: "Nifahari kuwa Kocha wa Nchi yangu na ni wadhifa wa kuvutia kama huu wa Chelsea ndio unaweza kufuatia huo!"
Guus Hiddink, ambae ndie Kaimu Meneja tangu Desemba alipofukuzwa Jose Mourinho, ataendelea na wadhifa huo hadi mwishoni mwa Msimu.
Conte, ambae alitwaa Ubingwa wa Italy wa Serie A katika kila Mwaka alipokuwa Bosi wa Juventus kwa Miaka Mitatu, anakuwa Mtaliana wa 5 kuwa Meneja wa Chelsea, kufuatia Gianluca Vialli, Claudio Ranieri, Carlo Ancelotti na Roberto di Matteo.
Kibarua kikubwa kwa Conte ni kuijenga upya kupigania Ubingwa wa England baada ya kuutwaa Msimu uliopita chini ya Mourinho na Msimu huu Timu kufanya ovyo kiasi ambacho imeshindwa kutetea Taji lao na hata kuwemo 4 Bora ni kitu kisisichowezekana.
 
Supported by AMAGA Media services : | |
Copyright © 2015. UKURASA WA HABARI - All Rights Reserved
Templete Designed by Abdallah Magana
Proudly powered by Blogger