MVUA ZAUA WATANO DAR,MAMIA HAWANA MAKAZI

 
Wananchi wakipita kwa shida katika Barabara ya Morogoro eneo la Jangwani jana baada ya kufurika maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha Dar es Salaam. Picha na Said Khamis 
 

  • Mvua hiyo iliyofikia kipimo cha milimita 132.5 kwa mujibu wa vipimo vilivyofanywa katika kituo cha Shule ya Msingi ya Maktaba, ilisababisha barabara kujaa maji na nyingine kuharibika na madaraja kadhaa kukatika.
 

Dar es Salaam. Mvua kubwa iliyonyesha kwa siku mbili mfululizo tangu juzi imesababisha vifo vya watu watano huku mamia wakikosa makazi baada ya nyumba zao kubomolewa.
Mvua hiyo iliyofikia kipimo cha milimita 132.5 kwa mujibu wa vipimo vilivyofanywa katika kituo cha Shule ya Msingi ya Maktaba, ilisababisha barabara kujaa maji na nyingine kuharibika na madaraja kadhaa kukatika.
Mkurugenzi Mkuu wa Hali ya Hewa, Dk Agnes Kijazi alisema jana kwamba kipimo hicho cha mvua ni cha juu mno kulinganisha na kile cha wastani ambacho ni kati ya milimita 16 na 30.
“Kwa takwimu za mwezi Mei, kiwango hiki hakijawahi kufikiwa kwa miaka 10 iliyopita.” Alipotakiwa kufafanua miezi mingine, Dk Kijazi alisema hakuwa na takwimu kwa kuwa alikuwa nje ya ofisi.
Awali, Dk Kijazi alitoa taarifa ikisema mifumo ya hali ya hewa inaonyesha kuwa “hali ya mvua inatarajiwa kuendelea katika baadhi ya siku hadi Mei 20, mwaka huu”.
“Mamlaka inaendelea kushauri wakazi wa maeneo hatarishi pamoja na watumiaji wa bahari kuchukua tahadhari,” alisema Dk Kijazi.
Watano wafa
Kutokana na mafuriko hayo, watu watano wakiwamo watoto wawili, walipoteza maisha baada ya kusombwa na maji.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick alisema waliopoteza maisha ni watoto wawili na mzee mmoja ambao majina yao hayajafahamika.
“Mtoto mmoja (2) alisombwa na mafuriko katika eneo Machimbo ya Makangarawe na mzee mmoja alifariki jana baada ya mvua kunyesha na kujaa ndani ya nyumba yake. Mtoto mwingine ambaye bado hajapatikana alisombwa na mafuriko pia,” alisema Sadick.
Hata hivyo, habari zilizopatikana wakati tunakwenda mitamboni zilisema kuwa waliopoteza maisha ni watu watano.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alimtaja mtu aliyefariki dunia kuwa ni Shabani Idd (73) mkazi wa Manzese.

 
Maeneo mengine
Katika eneo la Mbezi Luis, Mto Mbezi ulifurika, hali iliyosababisha nyumba zilizojengwa kandokando ya daraja hilo kufunikwa na maji.
Mkazi wa eneo hilo, John David alisema hali ilikuwa mbaya zaidi jana asubuhi kwani maji yalifurika na kujaa barabarani na kusababisha usumbufu mkubwa kwa watumiaji.
Alisema wakazi walio karibu na mto huo walichukua tahadhari tangu juzi na kuhama makazi yao.
“Haikuwa rahisi kwa wao kuendelea kukaa hapa wakati wanafahamu hali kama hii ingetokea. Tangu jana jioni familia zinazoishi huko ziliondoka, lakini vitu vyao vimesombwa na maji na nyumba moja imesombwa pia,” alisema David.
Maeneo ya Boko Basihaya, zaidi ya nyumba 20 zilikuwa zimezingirwa na maji huku familia kadhaa zikilazimika kukimbia nyumba zao na kutafuta makazi ya muda kuanzia juzi usiku hadi jana.
Timu ya waandishi wa Mwananchi ilifika katika eneo hilo na kushuhudia maji yakiwa yamejaa kwenye nyumba zilizojengwa kandokando ya bwawa linalotiririsha maji kuelekea baharini.
Mmoja wa wakazi wa eneo hilo, Dionise Swai alisema baada ya maji kujaa nyumbani kwake, alilazimika kuyanyonya kwa kutumia pampu ili kunusuru mali zake.
“Niliyawahi kwa hiyo hayakuingia. Wanafamilia wengine wameondoka nimebaki mwenyewe,” alisema.
Mkazi wa mwingine eneo hilo, Frank Shuma alizitupia lawama mamlaka kwa kushindwa kujenga mifereji ya kutiririsha maji kwenda baharini.
Hali kama hiyo pia ilitokea eneo la Kinondoni Hananasif ambako maji yalijaa na kufunika baadhi ya nyumba.
Katika daraja la Kawe, wananchi walikuwa kwenye harakati za kuokoa mali zao zilizosombwa na maji, yakiwamo magodoro, vyombo na nguo

Maji yalijaa kwenye barabara na kusababisha vyombo vya moto na watembea kwa miguu kupita kwa shida huku magari mengine yakilazimika kusimama pembeni.
Barabara ya Haile Selassie, upande wa baharini karibu na Hoteli ya Sea Cliff, eneo hilo lilifunikwa na maji na kusababisha usumbufu kwa vyombo vya moto na madereva kulazimika kuendesha kwa mwendo wa taratibu na kusababisha foleni.
Watumiaji wa barabara ya Mwai Kibaki walikuwa na wakati mgumu kupita, wengi walionekana wakiwa wamevua viatu au kutafuta njia mbadala kukwepa maji yaliyokuwa yamejaa barabarani.
Mkazi wa Ubungo Kibangu, Julieth Kibakaya alisema hofu imetanda kwa wakazi wa eneo hilo kutokana na athari zinazosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha hasa mafuriko.
“Huku kwetu hali ni mbaya. Mafuriko yamebomoa nyumba mbili hadi sasa. Hivi sasa wanafamilia hao hawana makazi tena imebidi wapewe hifadhi ya muda na majirani zao na hali ikiendelea hivi tunahofia wakazi wengi wa eneo hili watapoteza nyumba zao,” alisema Kibakaya.
CHANZO:MWANANCHI
.

MAGAZETI LEO IJUMAA




 

UCHAGUZI MKUU UINGEREZA KUFANYIKA KESHO

 
Wagombea nafasi ya waziri mkuu wa Uingereza

Viongozi wa vyama na wagombea wanafanya kampeni zao za mwisho kuwashawishi wapiga kura wawapigie kura kabla ya kufunguliwa uchaguzi mkuu.
Waziri Mkuu David Cameron ataahidi "kuifanya Uingereza kuwa katika njia ya mafanikio", wakati ambapo kiongozi wa chama cha Labour Ed Miliband ataahidi kuwa na "serikali itakayowajali kwanza wafanyakazi".
Kiongozi wa Lib Dem,Nick Clegg ataahidi hali ya utulivu.
Kura ya maoni inaonyesha hakuna chama kitakachoweza kushinda moja kwa moja kwa wingi wa viti.
Naibu mhariri wa BBC James Landale amesema wanasiasa, wapiga kura na vyombo vya habari wanajaribu kufuatilia kwa kina uchaguzi huo, na kuwafanya wengi kufuatilia kile kitakachotokea iwapo matokeo yatakuwa kinyume na matarajio yao.
"Alhamisi, huenda isiwe mwisho wa mchakato huo wa uchaguzi," amesema.
"Huenda uchaguzi huo ukaenda katika hatua ya pili baada ya kushindwa kumpata mshindi wa moja kwa moja."
Katika habari nyingine za uchaguzi mkuu:
Mgombea wa chama cha UK Independence Party (UKIP) aliondolewa katika kinyang'anyiro cha uchaguzi huo baada ya kupigwa picha akimtishia kumpiga risasi mpinzani wake kutoka chama cha Conservative.
Kiongozi wa Labour Ed Miliband amesema haamini kama chama chake kitakopa zaidi ya ilivyokuwa mipango ya chama cha Conservative iwapo kitashinda uchaguzi.CHANZO: BBC

CHADEMA: JK AACHE ''SAFARI ZA OVYO"

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe

KAMATI Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), imeazimia na kulaani tabia ya Rais Jakaya Kikwete kusafiri ovyo nje ya nchi wakati taifa lipo katika kipindi kigumu na matatizo makubwa ambayo yanahitaji uongozi thabiti.  
Kamati Kuu ilikutana kwa siku mbili kati ya tarehe 3 hadi 5 Mei mwaka huu, na kuitaka pia serikali kuchukua hatua za dharura kunusuru shilingi kwani athari zake ni kubwa sana kiuchumi na kijamii na kwamba zitasababisha mfumuko wa bei.
Akisoma maazimio hayo leo kwa waandishi wa habari katika Makao Makuu ya Chadema yaliyopo mtaa wa Ufipa Kinondoni, Katibu Mkuu wake, Dk. Willibrod Slaa, amesema kamati kuu vile vile ilipokea na kujadili hali halisi ya sekta ya usafirishaji nchini.
Amesema kuwa, wamebaini udhaifu mkubwa ambao upo ndani ya sekta hiyo kutokana na usimamizi dhaifu wa watu ambao walipewa dhamana kuanzia Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta ambaye ameshindwa kabisa.
“Hali hiyo inasababisha sekta hiyo kukosa mwelekeo na hivyo kuleta madhara mengi kwa wananchi kutokana na ajali za kila siku kuanzia vyombo vya majini na barabarani. Kamati kuu imebaini kutokana na mgomo wa madereva wananchi wameathirika kisaikolojia na kiuchumi,”amesema.
Kwa mujibu wa Dk. Slaa, Kamati kuu, imeazimia kuunga mkono madai ya madereva kwani ni halali na hivyo ni lazima serikali iyatekeleze madai yao yote ya muda mrefu. Amesema “kuendelea kuyapuuza ni kukubali kuendelea kuhatarisha maisha ya abiria.”
Kuhusu uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu, Dk. Slaa amesema kamati kuu imepokea taarifa ya kina namna ambavyo hadi sasa maandalizi ya msingi kisheria hayajafanyika. Ametaja kuwa ni mandalizi ya vifaa, fedha, kutangaza majimbo na kata mpya, kutangaza vituo na kusuasua kwa uandikishaji wapiga kura.
“Katika jambo hili, kamati kuu imeazimia kuwa uchaguzi huo lazima ufanyike Oktoba kwa mujibu wa Katiba na serikali ya CCM isijiandae kutumia kisingizio chochote kuahirisha kwa sababu uchaguzi sio jambo la dharura, bali lilijulikana miaka mitano iliyopita,” amefafanua.
CHANZO MWANAHALISI ONLINE

MGOMBEA URAIS CHADEMA KUPATIKANA AGOSTI 4


 Chadema Diaspora (Chadema or Die)
Viongozi wa Chadema wakiomba dua kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho kilichofanyika Dar es Salaam jana. Kuanzia kulia ni Makamu Mwenyekiti, Profesa Abdallah Safari, Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, Katibu Mkuu Dk Willibrod Slaa na Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar), Salum Mwalimu. Picha na Venance Nestory
Dar es Salaam. Kamati Kuu ya Chadema imepanga Agosti 4 kuwa siku ya kumpata mgombea wake wa urais ambaye ataingia kwenye kinyang'anyiro cha kumtafuta mgombea wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
Vyama vinne vilivyounda Ukawa, Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD, vimekubaliana kusimamisha mgombea mmoja wa kuanzia ngazi ya urais, lakini kila chama kitateua mgombea wake kabla ya kukubaliana mtu atakayeungwa mkono na vyama vyote.
Ratiba iliyotolewa jana na Chadema inaonyesha kuwa chama hicho kitatumia siku 76, kuanzia Mei 18, kumaliza mchakato wa kuwapata wagombea wake wa nafasi za udiwani, ubunge na urais kwa kuhitimisha na Mkutano Mkuu. Kwa mujibu wa ratiba hiyo, Chadema itampata mgombea wake wa urais takriban siku 14 zaidi kulinganisha na mwaka 2010 wakati Dk Willibrod Slaa alipoteuliwa.
Kwa mujibu wa Ibara ya 7.710 (C) ya katiba ya Chadema, Mkutano Mkuu ndiyo chombo chenye mamlaka ya kumpitisha mgombea wa urais kwa tiketi ya chama hicho.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe aliwaambia wanahabari jana kuwa kamati hiyo imeridhia mchakato wa uchukuaji na urejeshaji fomu uanze ili watia nia katika maeneo mbalimbali waanze kuchukua fomu za udiwani, uwakilishi na ubunge.
Katika ratiba hiyo , chama hicho kimeyapa kipaumbele maeneo yanayoonekana kutokuwa na madiwani na wabunge, kuanza kuchukua fomu siku ya kwanza ya kazi hiyo na kuzirudisha Juni 25.
Aidha ratiba hiyo inaonyesha kuwa makada waliopo kwenye maeneo yenye madiwani watachukua na kurejesha fomu ndani ya siku 10 kuanzia Julai Mosi.
Wakati huo, maeneo yenye wabunge kwa sasa yakipatiwa siku tano za kukamilisha uchukuaji na urejeshaji wa fomu hizo kuanzia Julai 6 hadi 10 huku vigogo wanaounyemelea urais wakipigiwa kipenga Julai 20 hadi 25.
Mara baada ya wagombea urais kukamilisha taratibu za kinyang'anyiro, Chadema imepanga kufanya uteuzi wa mwisho wa wagombea ubunge Agosti 1 na 2 huku Baraza Kuu likipangwa kukutana siku inayofuata kabla ya Mkutano Mkuu kukutana Agosti, 4.
Chadema imeungana na CUF kutangaza ratiba ya kuwapata wanachama watakaowania uongozi katika Uchaguzi Mkuu ambao kikatiba unatakiwa ufanyike wiki ya mwisho ya Oktoba na kubakiza mchakato wa kumpata mgombea mmoja kila nafasi ya uongozi.
Akielezea zaidi yaliyojiri katika vikao vya kawaida vilivyofanyika Mei 3 na 4 mwaka huu, Mbowe alisema Kamati Kuu ilipokea na kujadili makubaliano yaliyofikiwa ndani ya Ukawa.
Mbowe, ambaye pia ni mbunge wa Hai, alisema kuwa kamati hiyo iliwapongeza viongozi hao kwa hatua walizofikia na kuwataka wamalize masuala machache yaliyosalia ili wawajulishe Watanzania wanaounga mkono umoja huo wajue kinachoendelea.CHANZO: MWANANCHI 

MADEREVA WA VYOMBO VYA MOTO WAGOMA TENA LEO





Madereva wa Vyombo vya Usafirishaji katika maeneo mbalimbali  nchini, wameingia katika Mgomo tena leo kutotoa huduma hiyo kwa kile kinachodaiwa kwamba wanaitaka serikali iwasikilize madai ya mikataba yao kati yao na waajiri.
Hali ya mgomo huo, umepelekea adha kubwa kwa abiria wa vyombo hivyo, hasa wale waliokuwa wakielekea mikoani, pamoja na watu wenye magari yao kwani baadhi ya maeneo kama jijini Mbeya magari ya watu  binafsi yamelazimishwa kupandisha abiria tena bure na baadhi ya baiskeri ya matairi matatu hali maarufu kama bajiji na pikipiki zimeendelea kutoa huduma ya usafiri kwa bei ghari zaidi hali inayopelekea wasio na kipato kutembea kwa miguu kuelekea katika shughuri zao.
hali hii imesababisha abiria wengi wa daladala kutembea kwa miguu katika jiji hapa na baadhi ya abiri a katika stendi kuu ya mabasi jiji hapa kukosa usafiri hali inayosababisha hadha kwa abiria hao ambao wamejazana katika stendi hiyo na stendi ya nane nane hali kadhalika ni hivyo hivyo.

 


RATIBA YA LIGI KUU NCHINI ENGLAND KWA WIKIEND HII HIPO HAPA

 
 
RATIBA:
**Saa za Bongo
Jumamosi Mei 2
1445 Leicester v Newcastle
1700 Aston Villa v Everton
1700 Liverpool v QPR
1700 Sunderland v Southampton
1700 Swansea v Stoke
1700 West Ham v Burnley
1930 Man United v West Brom
Jumapili Mei 3
1530 Chelsea v Crystal Palace
1800 Tottenham v Man City
Jumatatu Mei 4
2200 Hull v Arsenal 
 
 
 
Jumamosi Mei 9
1445 Everton v Sunderland
1700 Aston Villa v West Ham
1700 Hull v Burnley
1700 Leicester v Southampton
1700 Newcastle v West Brom
1700 Stoke v Tottenham
1930 Crystal Palace v Man United
Jumapili Mei 10
1530 Man City v QPR
1800 Chelsea v Liverpool
Jumatatu Mei 11
2200 Arsenal v Swansea
Jumamosi Mei 16
1445 Southampton v Aston Villa
1700 Burnley v Stoke
1700 QPR v Newcastle
1700 Sunderland v Leicester
1700 Tottenham v Hull
1700 West Ham v Everton
1930 Liverpool v Crystal Palace
Jumapili Mei 17
1530 Swansea v Man City
1800 Man United v Arsenal
Jumatatu Mei 18
2200 West Brom v Chelsea
Jumatano Mei 20
2145 Arsenal v Sunderland
Jumapili Mei 24
**Mechi za mwisho za Ligi
**Zote  kuanza Saa 1700
Arsenal v West Brom
Aston Villa v Burnley
Chelsea v Sunderland
Crystal Palace v Swansea
Everton v Tottenham
Hull v Man United
Leicester v QPR
Man City v Southampton
Newcastle v West Ham
Stoke v Liverpool
 
 

MANY PACQUIAO ASEMA HAYA KUELEKEA MPAMBANO WA MASUMBWI

UKAWA YAKATAA MIZENGWE YA NEC


Viongozi wa Vyama vinavyounda Umoja wa wadai Katiba ya wananchi (UKAWA), Freeman Mbowe (kushoto), James Mbatia (katikati), Prof. Ibrahim Lipumba (wa pili kulia) na Dk. Emmanuel Makaidi
Viongozi wa Vyama vinavyounda Umoja wa wadai Katiba ya wananchi (UKAWA), Freeman Mbowe (kushoto), James Mbatia (katikati), Prof. Ibrahim Lipumba (wa pili kulia) na Dk. Emmanuel Makaidi

VYAMA vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) leo vimetoa msimamo juu ya njama za kuahirisha uchaguzi mkuu unaotakiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.  

Msimamo huo wameutoa katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
UKAWA imesisitiza kwamba kuahirisha Uchaguzi Mkuu ni sawa na kumuongezea  Rais Jakaya Kikwete na Chama cha Mapinduzi (CCM) muda wa kuendelea kutawala.
UKAWA imesema jaribio lolote la kuahirisha Uchaguzi Mkuu kwa kisingizio chochote kile litakuwa kinyume na Katiba ya sasa ya Tanzania na litahesabika sawa na Mapinduzi dhidi ya Katiba.
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF, Profesa Ibrahim Lipumba amesema ” Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) haijaanza maandalizi yoyote kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu licha ya kwamba imebaki miezi sita tu Uchaguzi Mkuu ufanyike kwa mujibu wa Katiba”.
Lipumba amesema shughuli zinazohusiana na maandalizi ya Uchaguzi Mkuu na vifaa vinavyotumika Kwa ajili yake ambavyo kwa taratibu za  miaka yote huanza kufanyika angalau mwaka mmoja na nusu kabla ya siku ya uchaguzi hazijaanza kufanyika, vifaa vinavyoohitaji havijanunuliwa na fedha kwa ajili hiyo hazijategwa hadi sasa.
Aidha, Lipumba amesema “Licha ya madai ya muda mrefu ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kwamba ratiba ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 imevurugwa kwa makusudi kwa kutokutenga Fedha kwa ajili hiyo katika bajeti ya serikali tangu mwaka 2012″.
“Serikali ya CCM haijatoa fedha kwa NEC kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu. Badala yake NEC imeendelea kutangaza kwamba inafanya maandalizi kwa ajili ya Kura ya Maoni kuhusu Katiba Inayopendekezwa ambayo imepitwa muda kisheria, “amesema Lipumba.
Hivyo Kwa Sheria ya Kura ya Maoni ilivyo kwa sasa, hakuna uwezekano wa Kura ya Maoni kufanyika tena bila kwanza kufanya marekebisho ya sheria hiyo.
Hadi sasa Serikali haijapeleka bungeni Muswada wa Sheria kurekebisha Sheria hiyo ili kuwezesha Kura ya Maoni.
Aidha, Mwenyekiti wa chama cha NCCR  – Mageuzi, James Mbatia amesema “kuruhusu Uchaguzi Mkuu uahirishwe kwa kisingizio chochote ni kuwazawadia wazembe na kuwaongezea mafisadi wanaolimaliza taifa kwa ufisadi muda wa kuendelea na ufisadi”.
” Watu hawa wanafahamu kuwa tumekuwa tukifanya Uchaguzi Mkuu kila baada ya miaka mitano tangu mwaka 1960. Hata mwaka 1980, miezi michache baada ya kutoka vitani dhidi ya Nduli Iddi Amin wa Uganda na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere kutangaza miezi 18 ya kujifunga mikanda kwa sababu ya hali mbaya ya uchumi iliyosababishwa na vita ya Uganda, hatukuahirisha Uchaguzi Mkuu wa mwaka huo, “amesema Mbatia.
Mwenyekiti wa chama cha National League for Democracy (NLD), Dk. Emmanuel Makaidi amesema “kubadilisha Katiba ya salsa kwa lengo la kuahirisha Uchaguzi Mkuu wa Oktoba sio tu kutaathiri misingi muhimu ya Katiba ya sasa, bali pia kutahatarisha amani ya nchi”.
“Tumeona kinachoendelea Burundi baada ya Raid Pierre Nkurunzinza na chama chake kuamua kuamua kujiongezea muda wa kutawala nchi hiyo. Tumeona yanayoendelea Jamhuri ya Kidemokrasia ya  Congo (DRC) baada ya Joseph Kabila kutaka kufanya hivyo. Kikwete na wanaCCM wenzake wasitake kuingiza nchi yetu katika majanga yasiyokuwa na sababu,” ameongeza Makaidi.
Aidha, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amesema “Tume iliwaahidi watanzania kwamba watu wote wenye sifa wataandikishwa katika Daftari la Wapiga Kura”.
“Leo Tume inapunguza muda wa siku 14 hadi siku 7 wakati tunafahamu kwamba Tume inavifaa pungufu vya kuandikisha wapiga kura. Hii ni njama ya Tume na serikali kuhakikisha wapiga kura wengi hawaandikishwi,” amesema Mbowe.
Kuhusu mgawanyo ndani ya majimbo. UKAWA imesema kati ya majimbo 239 nchi nzima, tayari wamekubaliana majimbo 227 huku majimbo 12 bado yakiwekewa vigezo kwa ajili ya kugawana.
UKAWA imekana taarifa zilizosambazwa na baadhi ya vyombo vya habari kuhusu “chama cha NCCR – Mageuzi kimejitoa au kimeandika barua ya kuomba kujitoa kwenye UKAWA.

Mayweather thanks God, acknowledges the Filipinos for rallying behind wo...

 
Supported by AMAGA Media services : | |
Copyright © 2015. UKURASA WA HABARI - All Rights Reserved
Templete Designed by Abdallah Magana
Proudly powered by Blogger