JOHAN CRUYFF AFARIKI DUNIA


 

Johan Cruyff (kulia) akiwa na Mtendaji Mkuu wa BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE, Mahmoud Zubeiry enzi za uhai wake alipozuru Tanzania mwaka jana PICHA ZAIDI GONGA HAPA

HISTORIA YA JOHAN CRUYFF 

MCHEZAJI 
Ajax (1964-73) – Mechi 240 mabao 190 
Barcelona (1973-78) – Mechi 143 mabao 48 
LA Aztecs (1979-80) – Mechi 23 mabao 13 
Washington Diplomats (1980-81) – Mechi 30 mabao 12
Levante (1981) – Mechi 10 Mabao 2 
Ajax (1981-83) – Mechi 36 Mabao 14 
Feyenoord (1983-84) – Mechi 33 Mabao 11 
Uholanzi (1966-77) – Mechi 48 Mabao 33 
 
KOCHA
Ajax (1985-88)
Barcelona (1988-96)
Catalonia (2009-13)
GWIJI wa soka, Mholanzi Johan Cruyff amefariki dunia akiwa ana umri wa miaka 68.
Cruyff, ambaye aliichezea mechi 48 Uholanzi pamoja na klabu za Ajax ya kwao na Barcelona ya Hispania, amefariki dunia leo baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa saratani.
Taarifa katika tovuti yake imesema; "Machi 24 mwaka 2016 Johan Cruyff (miaka 68) amefariki dunia kwa amani mjini Barcelona, akiwa amezungukwa na famili yake baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa saratani,".
"Ilikuwa ni huzuni kubwa na tunakuomba uheshimu siri za familia katika wakati huu mgumu,".
Cruyff,ambaye ameshinda mataji matatu ya Ulaya na manane ya Uholanzi akiwa na Ajax, ameanza kusumbuliwa na saratani tangu Oktoba mwaka jana.
Aprili mwaka jana, Cruyff alizuru Tanzania pamoja na kikosi cha Maveterani wa Barcelona ambao walicheza mechi ya wachezaji wa zamani nchini Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

STARS NA CHAD KATIKA PICHA JANA



Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mbwana Samatta (kulia) akipambana na beki wa Chad katika mchezo wa Kundi G, kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika 2017 jana Uwanja wa Omnisports Idriss Mahamat Ouya mjini D'jamena. Taifa Stars ilishinda 1-0

Mshambuliaji wa Taifa Stars, Mbwana Samatta akimvisha kanzu ya kisigino watoto wa bongo wanasema 'kizungu' beki wa Chad jana

Mshambuliaji wa Taifa Stars, Thomas Ulimwengu akigombea mpira na beki wa Chad jana

Winga wa Taifa Stars, Farid Mussa akimtoka beki wa Chad jana

Kiungo wa Taifa Stars, Mwinyi Kazimoto akitafuta maarifa ya kuwapita wachezaji wa Chad jana

Beki wa kulia wa Taifa Stars, Shomary Kapombe (kushoto) akitafuta maarifa ya kumpira beki wa Chad jana

Mshambuliaji wa Tanzania, Thomas Ulimwengu akimruka kipa wa Chad baada ya kudaka mpira

Kiungo wa Taifa Stars, Jonas Mkude akimtoka mchezaji wa Chad huku akifikiria pia namna ya kumpita mchezaji mwingine wa timu hiyo jana

Kiungo wa Taifa Stars, Himid Mao (kulia) akiwania mpira dhidi ya mshambuliaji wa Chad jana 

Kikosi cha Taifa Stars kilichlifunga 1-0 Chad jana mjini D'jamena

Ndege yakamatwa ikisafirisha Nyani

Habari niliyoipokea muda mfupi uliopita zinamhusu Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof Jumanne Magembe kumsimamisha kazi Mkurugenzi msimamizi wa wanyama pori  Charles Mulokozi kwa kutoa vibali vya kusafirisha wanyama kwenda nje pamoja na wakurugenzi wanne wa Huduma za misitu kutokana na usafirishaji na uvunaji  holela wa magogo.
Akizungumza na kituo cha ITV Waziri Magembe amesema….>>>watu wanavuna mazao ya misitu kule kalambo, tukaenda kule tukakutana na  magogo mengi sana yako msituni ambayo yanatakiwa yawe yamelipiwa na hayakulipiwa, nimewaondoa hili tuweke uongozi mpya kwa sababu kinachoonekana ni kwamba hawana uwezo wa kuongoza’
Kuhusu kumsimamisha kazi Mkurugenzi msimamizi wa wanyama pori  Charles Mulokozi, Waziri Magembe amesema .…..>>>Jana usiku tumekamata ndege ambayo ilikuwa inasafirisha nyani, inaonekana ni biashara inayofanywa kwa hiyo amesimamishwa kazi, uchunguzi ufanywe ili tuone hili jambo la kusafirisha wanyama nje ya nchi limefanywa kiasi gani na ni nani anafanya’

Wafahamu Wabunge wapya walioteuliwa na NEC

 

LADY JAYDEE MEDIA TOUR LEO NI RADIO ONE

KIKOSI KAMILI CHA STARS DHIDI YA CHAD LEO HIKI HAPA



Kikosi cha leo cha Taifa Stars dhidi ya Chad, mzigo kamili huu hapa...

1. Aishi Manula
2. Shomari Kapombe
3. Haji Mwinyi
4. Erasto Nyoni
5. Kelvin Yondani
6. Himid Mao
7. Jonas Mkude
8. Mwinyi Kazimoto
9. Mbwana Samatta
10. Thom Ulimwengu
11. Farid Mussa

Sub:
Ally Mustapha
Mohammed Hussein
David MWantika
Shiza Kichuya
Ibrahim Ajib
John Bocco

UKAWA Washinda Umeya wa jiji la Dar es Salaam



    
Hatimaye uchaguzi wa Meya wa jiji la Dar es Salaam umekamilika leo katika ukumbi wa Karimjee, na kushuhudia Isaya Mwita wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) akitangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi huo.
Mwita ameibuka na ushindi na kutangazwa kuwa Meya Mpya wa Jiji la Dar es Salaam baada ya kupata kura 84 akimshinda mpinzani wake, Yenga Omary  wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) aliyepata kura 67.
Uchaguzi huo umeweka historia ambapo kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi (1992), Chama Cha Upinzani kimepata nafasi ya kuongoza jiji hilo.
Uchaguzi huo uliahirishwa mara kadhaa kutokana na mvutano uliokuwa unaibuka kati ya wajumbe wa CCM na Chadema na kuzua vurugu wakati mwingine.
Tofauti na ilivyo kwa tarehe nyingine za uchaguzi zilizopangwa na kuahirishwa wakati wajumbe wakiwa ukumbini, viongozi wa ngazi za juu wa Chadema pamoja na aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya chama hicho, Edward Lowassa walihudhuria kushuhudia uchaguzi huo.

TAIFA STARS WANAVYOJIFUA NCHINI CHAD WAKIWASUBIRI WENYEJI KESHOKUTWA


Kikosi cha Taifa Stars kimeendelea kujifua mjini N’Djamena kikiwasubiri wenyeji Chad, keshokutwa.

Stars inaivaa Chad katika mechi ya kuwania kucheza Kombe la Mataifa Afrika, huku ikiwa na matumaini makubwa.



Nahodha wake, Mbwana Samatta ndiye aliyekuwa wa kwanza kuwasili Chad akitokea Ubelgiji ambako anakipiga katika klabu ya KRC Genk.


Hata hivyo, bado kundi moja litajiunga na wenzao kesho akiwemo Thomas Ulimwengu ambaye anatokea DR Congo ambako anaitumikia klabu ya TP Mazembe.



HII NDIO NDEGE NDEFU NA KUBWA ZAIDI DUNIANI

Ndege hiyo inayojulikana kama (The Airlander 10) ina urefu wa mita 92 ikiwa ni mita 18 zaidi ya urefu wa ndege ya kawaida.
 Comparison of Airlander 10 to an airplane.
Kampuni moja ya uingereza imechukua miaka 9 kuijenga ndege hiyo katika kiwanda kikubwa zaidi cha ndege cha Cardington kilicho eneo la Bedfordshire

 Airlander-10-640x450

Ndege hiyo iliyogharimu dola milioni 25 kuijenga inaweza kusimama eneo moja hewani kwa wiki tatu na na pia inaweza kuendelea kuruka hata baada ya kutobolewa mashimo kwa njia ya risasi.
Jeshi la Uingereza liliishiwa na pesa za kumaliza ujenzi wake kuitumia kama ndege yao ya ujasusi hali iliyosababisha kampuni ya huduma za ndege ya Uingereza kujitwika jukumu la kuikamilisha.
Wengi wanaamini kuwa ndege hiyo isiyo na kelele ikiwa angani wa isiyotoa hewa chafu inaweza kutumiwa kwa usafiri siku za usoni.

Magazeti ya leo jumapili March 20,2016

 20160320_051519
20160320_051533
20160320_051549
20160320_051600
20160320_051614
20160320_051623
20160320_051636
20160320_051646
20160320_051704
20160320_051717
20160320_051730
20160320_051744
20160320_051756
20160320_051808
20160320_051818
20160320_051832
20160320_051845
20160320_051858
20160320_051910
20160320_051921
20160320_051932
20160320_051942
20160320_052011
20160320_052026
20160320_052040
20160320_052103
20160320_052126
20160320_052138
 
 
Supported by AMAGA Media services : | |
Copyright © 2015. UKURASA WA HABARI - All Rights Reserved
Templete Designed by Abdallah Magana
Proudly powered by Blogger