Van Gaal:CHICHARITO KUBAKI OLD TRAFFORD, STRAIKA MWINGINE KUTINGA!

    48AB9AF646274007A4766CAD8F13941A                                                                                                                                                             Louis van Gaal amekiri Javier Hernandez 'Chicharito' atapata nafasi nyingine ya kupigania nafasi yake kwenye Kikosi cha Manchester United akiungana na Timu hiyo hapo Julai 25 huko Ziarani Marekani.
    Chicharito, ambae aliifungia Man United Bao 59 katika Mechi154, alipelekwa kwa Mkopo huko Real Madrid Msimu uliopita baada Van Gaal kuamua atakuwa nyuma ya Wayne Rooney, Robin van Persie na Radamel Falcao katika kupewa namba.
    Lakini, baada ya Man United kuifunga Club America 1-0 mapema Leo, Van Gaal aliulizwa hatima ya Chicharito na kueleza: "Chicharito anakuja Julai 25. Ana nafasi ya kudhihirisha uwezo wake hasa baada ya Falcao na Van Persie kuondoka, hivyo nafasi yake kubwa."
    Hivi sasa Man United imebakiwa na Mastraika Wawili tu wanaotambulika ambao ni Kepteni Wayne Rooney na James Wilson na alipoulizwa kuhusu upungufu huo, Van Gaal alijibu: "Hapana tunae Rooney anaweza kucheza kama Straika mkuu. Wanahabari wote Msimu uliopita waliandika anapaswa kucheza hapo na mimi nawasikiliza. Na tunae Chicharito, na labda Wilson, na pengine kwa kushangaza..mpya., huu ni mchakato. Sina wasiwasi na nafasi hiyo."

    Raw: Wildfire Sweeps Over CA Freeway, Burns Cars



    Cars are shown burning on the Interstate 15 freeway in the Cajon Pass, California in the frame grab from KNBC video July 17, 2015.  A brush fire burning in foothills north of Los Angeles overran a freeway in a mountain pass on Friday, torching several cars and trucks as drivers scrambled to safety.  REUTERS/NBCLA.COM/HANDOUT  FOR EDITORIAL USE ONLY. NOT FOR SALE FOR MARKETING OR ADVERTISING CAMPAIGNS  NO SALES NO ARCHIVES       TPX IMAGES OF THE DAY


    Kama unasafiri kwenye barabara kubwa kama ya Dar-Mbeya, au Dar-Mwanza au
    barabara yoyote kubwa ya magari njiani kuna vibao vya tahadhari kwamba
    usiwashe moto.. ule moto athari yake sio kwenye misitu pekeake, noma
    inaweza kuhamia hata barabarani !!
    0
    July 17 2015 barabara kuu ya
    California-Las Vegas Marekani wameshuhudia hili tukio, moto ulikuwa
    unawaka tu vichakani.. upepo mkali ukausukuma ule moto mpaka
    barabarani.. kulikuwa na magari ambayo hayakupona kabisa, yameshika moto
    na kuishia hapohapo japo watu wa Zimamoto walijitahidi kuzima kwa
    kisasa kabisa kutumia Helicopter lakini sio gari zote zilizopona.
    wild-fire
    Madereva wa magari na watu waliowabeba
    wakaona hili sasa balaa, ikabidi wayaache magari na kukimbia..
    kilichotishia watu sio moto pekeake, kulikuwa na milio ya milipuko
    mikubwa ambayo ilitokana na matairi ya gari kupasuka.
    Zaidi ya magari 20 yameungua kwa moto,
    mengine yalitelekezwa na watu waliokimbia.. na kuna wengine ilibidi
    wageuze kurudi walikotoka ili kujiokoa… hakuna taarifa kama kuna mtu
    yoyote aliyefariki ila kuna majeruhi ambao ni watu wawili tu.
    2380
    AP_California_Wildfire_150718_DC_16x9_992
    Hali ilikuwa mbaya kiasi cha kusababisha hata barabara kufungwa… Hiyo story iko na kwenye Video hapa.
                                                                     



    MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI JULLY 18,2015 HAYA HAPA

     
    DSC09743

    DSC09743 DSC09744 DSC09745 DSC09746 DSC09747 DSC09748 DSC09749 DSC09750 DSC09751 DSC09752 DSC09753 DSC09754 DSC09755 DSC09756 DSC09757 DSC09758 DSC09759 DSC09760 DSC09761 DSC09762 DSC09763 DSC09765 DSC09766 DSC09767 DSC09768 DSC09771

    BENITEZ: RAMOS ANABAKI SANTIAGO BERNABEU!

    SERGIO-RAMOS

                                                                                                                                                                                      Meneja mpya wa Real Madrid Rafael Benitez ametoboa kuwa Beki wao Sergio Ramos hatahama.
    Mwezi Juni Manchester United ilitoa Ofa ya Pauni Milioni 28.6 kumnunua Beki huyo wa Kimataifa wa Spain na Ofa hiyo kugomewa na Real.
    Hivi sasa Man United wanaisuka upya Timu yao chini ya Meneja Louis van Gaal na tayari wameshanunua Wachezaji wapya Wanne, ambao ni Viungo Bastian Schweinsteiger na Morgan Schneiderlin, Fulbeki wa Kulia Matteo Darmian na Winga Memphis Depay, huku Robin van Persie na Nani wakiiuzwa kwa Klabu ya Uturuki Fenerbahce.
    Ilitarajiwa Sergio Ramos atatua Man United huku Kipa wao David De Gea akienda Real lakini inaelekea Dili hii imekwama huku kila upande uking'ang'ania matakwa yake.
    Lakini Wachambuzi wengi walikuwa na imani kuwa nia halisi ya Ramos si kuhama Real bali kuishinikiza Klabu hiyo iboreshe Mkataba wake.
    Nao Man United hawana nia yeyote ya kumuuza David De Gea na wako tayari kukaa nae hadi mwishoni mwa Msimu ujao ambapo Mkataba wake utakapoisha na aondoke bure tu.
    Hata hivyo zipo pia habari kuwa ikiwa De Gea ataondoka hivi sasa basi Man United inataka ilipwe si chini ya Pauni Milioni 33 ili kumfanya Kipa huyo awe wa Bei ghali katika Historia na kupiku Dau ambalo Juventus lilitoa kumnunua Kipa wao Gianluigi Buffon kutoka Parma Mwaka 2001 walipolipa Pauni Milioni 32.1
    Akiongea kuhusu Ramos, ambae Real wamesafiri nae kwenye Ziara yao huko Australia, Benitez amesema: "Mengi yamezungumzwa kuhusu Ramos. Kwangu mimi Rais ashatamka anabakia Real. Namuona Ramos kama sehemu muhimu ya mipango yetu hapa Real. Yeye ni mshindi na hilo ndio tunataka kwa Timu yetu. "

    New Video: B.O.B Micharazo ~ Kazi Kwanza

     



    Haya
    kazi nyingine hii kutoka kwa B.O.B Micharazo, Audio imefanywa na Marco
    Chali na Video imefanywa na Adam Juma. Enjoy Mziki Mzuri kutoka kwa B.OB
    Micharazo.
                                                          

    Tazama Matokeo ya kidato cha sita 2015


     Akitangaza matokeo hayo mjini Zanzibar leo, Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde alisema mwaka huu idadi ya ufaulu ni asilimia 98.87 ikilinganishwa na asilimia 98.26.
    Na Mwandishi Wetu, Mwananchi
    Zanzibar. Baraza la Mitihani nchini Necta leo limetangaza matokeo ya mitihani ya kidato cha sita na kusema kuwa umefaulu umeongezeka kwa asilimia 0.61.
    Akitangaza matokeo hayo mjini Zanzibar leo, Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde alisema mwaka huu idadi ya ufaulu ni asilimia 98.87 ikilinganishwa na asilimia 98.26.
    Dk Msonde alisema jumla ya watahiniwa 38,853 wamefaulu mitihani hiyo kati ya watahiniwa 40,753 waliofanya mitihani hiyo ya kumaliza kidato cha sita. Aliongeza kuwa kuna watahiniwa 35 ambao walishindwa kufanya mitihani yao baada ya kuugua ghafla. Dk Msonde aliongeza kuwa kati ya waliofaulu, wasichana ni 11,734 na wavulana ni 27,119.


    MAGAZETI YA LEO JUMATANO JULY 15,2015 HAYA HAPA


    DSC00609 DSC00610 DSC00611 DSC00612 DSC00613 DSC00614 DSC00615 DSC00616 DSC00617 DSC00618 DSC00619 DSC00620 DSC00621 DSC00622 DSC00623 DSC00624 DSC00625 DSC00626 DSC00627 DSC00628 DSC00629 DSC00630 DSC00631 DSC00632 DSC00633 DSC00634 DSC00635 DSC00636 DSC00637 DSC00638 DSC00639 DSC00640 DSC00641
     
     
    Supported by AMAGA Media services : | |
    Copyright © 2015. UKURASA WA HABARI - All Rights Reserved
    Templete Designed by Abdallah Magana
    Proudly powered by Blogger