Kingunge anusa mchezo mchafu urais ndani ya CCM

 
Mwanasiasa mkongwe na kada wa CCM, Kingunge Ngombare Mwiru
Mwanasiasa mkongwe na kada wa CCM, Kingunge Ngombare Mwiru (Pichani) amesema anahisi kuna mchezo mchafu unapangwa kwenye mchakato wa kupata mgombea wa urais wa chama hicho tawala, akitaja idadi kubwa ya waliojitokeza kuwa ni ishara mbaya.
Mwanasiasa huyo mkongwe aliyefanya kazi na marais wa awamu zote nne, pia, bila kumtaja jina, alitumia muda mwingi kwenye hotuba yake kujibu kauli ya makamu mwenyekiti wa CCM, Phillip Mangula aliyekaririwa akisema kuwa mgombea wa chama hicho hatakiwi kujinadi.
Kingunge, ambaye amejitokeza hadharani kumpigia debe Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa alionyesha hofu hiyo jana wakati mbunge huyo wa Monduli alipokuwa akihitimisha kazi ya kusaka wadhamini mkoani Dar es Salaam kwenye ofisi za CCM Mkwajuni wilayani Kinondoni.(P.T)
Hadi sasa, makada waliochukua fomu kuwania urais kwa tiketi ya CCM ni 41 baada ya mwanachama mmoja kuchukua fomu jana akisema atamudu kupata wadhamini kwa njia ya mtandao katika siku tano zilizosalia. Akizungumza katika mkutano wa kusaka wadhamini ulioandaliwa kwa ajili ya Lowassa wilayani Kinondoni jana, Kingunge alipingana na kauli ya Mangula kuwa mgombea wa CCM atanadiwa na chama, si kujinadi mwenyewe akisema chama hicho kinataka mgombea anayekubalika ndani na nje.
Siku tatu zilizopita, Mangula alihojiwa na kituo cha televisheni cha Shirika la Utangazaji Tanzania(TBC) na kusema mgombea wa chama hicho hatakiwi kujinadi mwenyewe, kusisitiza kuwa anatakiwa kunadiwa na chama.
Lakini Kingunge aliikosoa kauli hiyo jana akisema chama hicho kimeweka utaratibu na hakuna sababu ya kuuacha na kuanza kuwahukumu wagombea kabla ya vikao na kusisitiza kuwa CCM haikuwahi kuwahukumu wagombea kabla katika chaguzi zilizopita.
“Mchakato ufuate taratibu zilizowekwa,” alisema Kingunge ambaye aliibuka Kinondoni ambako Lowassa alimalizia shughuli zake jijini Dar es Salaam.
“Nimemsikia kiongozi wetu mmoja tena juzi juzi hapa, nikamuona kwenye televisheni anasema mtu hawezi kwenda kujinadi yeye binafsi, ananadiwa na chama.
“Nikasema eh! hilo hilo. Lakini nataka nimweleze yeye na wenye fikra kama hizo kuwa kuna ngazi mbili katika utaratibu wetu; kwanza, mwanachama anayetaka kuwania ubunge, udiwani, urais lazima ajinadi ndani ya chama, ndivyo tulivyofanya miaka yote kwa mujibu wa katiba na taratibu zetu. Ndivyo wanavyofanya sasa wakina Lowassa.”
Alisema pili, wagombea wakishajinadi chama kitamteua mmoja ambaye kitamnadi na yeye ataendelea kujinadi.
“Si vizuri watu ambao tumewapa vyeo katika chama wakaanza ama wakaendelea kukitumia chama chetu kwa mambo yao binafsi. Kama wana mashaka tupo tunaojua mambo ya chama,” alisema Kingunge huku akishangiliwa na mamia ya watu.
Kingunge alisema mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwa Dodoma alisema chama kinatafuta mgombea anayekubalika ndani na nje ya chama hicho ili kuweza kushindana na vyama vingine.
“CCM inamtafuta mtu ambaye anakubalika ndani na nje ya chama. Wale wanaofanya jitihada za kuunda mazingira ya kukitafutia chama kushindwa, wanataka historia iliyotukuka ya CCM iishe katika awamu ya nne,” alisema.
”Tunapozungumzia suala la urais kwa sababu linahusu watu, tusianze kukaa kwenye mizengwe. Kwanza tuwaulize watu wanamtaka nani atayeweza kuwatatulia matatizo yao.”
Kingunge alisema idadi ya wagombea nafasi ya urais waliojitokeza kwa tiketi ya CCM ni wengi na kwamba idadi hiyo ambayo alisema haijapata kutokea katika historia ya chama, inaashiria kuwa kuna jambo linataka kufanyika.
“Nasema hao wagombea wapo wengi, sasa wenye macho wanaona watu wanasema nini. Matumaini yangu ni kwamba watu watatuliza vichwa kukubali ukweli na kuachia utaratibu wetu uendelee unavyotakiwa,” alisema.
Aliwataka viongozi ndani ya CCM kutokiuka taratibu za chama hicho za kumteua mgombea, kuwataka kutumia utaratibu uliozoeleka na ambao ulitumiwa katika chaguzi zilizopita.
Alisema Watanzania wana changamoto nyingi na kwamba tangu mwanzo chama hicho kimekuwa kikilia na umasikini unaolikabili taifa, huku akisisitiza kuwa mwarobaini wa kuondoa hali hiyo ni Lowassa.
Kingunge alisema licha ya marais wa awamu zote kufanya mambo mengi, nchi kwa sasa inahitaji kiongozi atakaye ondoa umaskini.
“Na linawezekana hilo, nasema tunapozungumzia suala zima la urais tunazungumzia hatma ya Watanzania. Tusifanye mchezo nalo, hatuwezi kukaa tukasema yeyote tu anaweza. Hiyo sio lugha ya watu makini. Kauli hiyo itasemwa na walionacho, lakini wasionacho hawawezi kusema hivyo,” alisema Kingunge.
Kauli ya Lowassa
Akizungumza kwa nyakati tofauti akiwa wilayani Ilala, Temeke na Kinondoni jijini Dar es Salaam, Lowassa alirejea kauli iliyotolewa na Mwalimu Julius Nyerere ya mwaka 1995, kwamba watu wanataka mabadiliko na wakiyakosa ndani ya CCM, watayatafuta nje ya chama hicho.
“Mimi nitayaleta haya mabadiliko nikiwa ndani ya CCM. Nagombea urais kwa sababu nauchukia umasikini na nitaunda serikali ya kusaidia wanyonge, kuwafukuza machinga, mamantilie na waendesha bodaboda ni upuuzi. Watu wanatafuta riziki tunawafukuza inatakiwa tuwawekee mazingira mazuri,” alisema na kushangiliwa kwa nguvu.
Alisema anauchukia msongamano wa magari jijini Dar es Salaam na iwapo atakuwa Rais atalimaliza tatizo la foleni katika jijini Dar es Salaam kwa miezi sita.
“Kutakuwa na waziri anayeshughulika na jiji la Dar es Salaam tu kama ilivyo kwa nchi jirani ya Kenya. Yeye akiamka tu akili yake yote ni kushughulikia changamoto za jiji hili,” alisema Lowassa ambaye mara kwa mara alikuwa akiwaimbisha wananchi wimbo wa ‘mchakamchaka’, huku akisisitiza kuwa ataiongoza serikali yake kwa mtindo wa mchakamchaka akisema ambaye hataweza atakaa pembeni.
Aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika Daftari la Wapigakura ili wapate fursa ya kumchagua iwapo atapitishwa na chama hicho kugombea urais, huku akiwataka wamuombee kwa maelezo kuwa Mungu ndiye anayepanga kila kitu.
“Mrema (Augustine) alikuwa maarufu sana mwaka 1995 mpaka gari lake likawa linasukumwa na wananchi, lakini katika kura za urais hakushinda. Jiandikisheni ili tufanikishe safari ya matumaini,” alisema.
Lowassa alisema kutokana na idadi kubwa ya wananchi wanaomuunga mkono anaona kama tayari ameshashinda huku akisisitiza kuwa ameshawafunga goli wagombea wenzake kama anavyofanya mchezaji wa timu ya soka ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo.
“Kati ya wagombea wote hakuna mwenye uzoefu ndani ya CCM kama mimi. Kumbukeni rais ndiye mwenyekiti wa CCM,” alisema.
Aiteka Dar
Lowassa aliwasili katika uwanja wa ndege wa zamani (Terminal 1), saa 2:00 asubuhi akitokea mkoani Arusha.
Mwenyekiti wa CCM wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida alisema wanachama wa mkoa huo waliojitokeza kumdhamini ni 212,150, kati yao kutoka Kinondoni ni 95,251, Temeke (72,100) na Ilala (44,799).
Afananishwa na mtume, Yesu
Akimkaribisha Lowassa Dar es Salaam, Madabida alimfananisha waziri mkuu huyo wa zamani na Mtume Muhammad ambaye alikuwa akitangaza dini lakini alikuwa akipingwa na watu wake wa karibu na kufafanua kuwa kutokana na hali hiyo Mungu alimueleza kuwa hatamuacha na atakuwa pamoja naye.

MAGAIDI WAKAMATWA MOROGORO

Breaking                                            Ripoti hii ni ya ITV June 27 2015 kutoka Morogoro inahusu watu watatu kufariki katika mapambano na Polisi, huku wawili kati yao wakihisiwa kuwa na uhusiano na kundi la kigaidi la Al Shabaab.
Breaking News nyingine kuhusu tukio hilihili iliyoripotiwa na Gazeti la Mwananchi inahusu watu sita kukamatwa na wengine 50 wanatafutwa, walikutwa wakiwa na sare za majeshi pamoja na silaha kama majambia kwenye msitu Mvomero.
Kwenye taarifa iliyofatia kutoka Mwananchi, imesema Mkulima Cassian Peter amefariki mchana wa June 27 2015 kwenye Hospitali ya Bwagala ambapo Polisi mmoja amelazwa na hii ni baada ya kujeruhiwa na hao watuhumiwa wa Ugaidi kabla hawajakamatwa.
ITV
Moro 1
Mtangazaji na Mwandishi wa habari wa Radio One Maulid Kambaya kwenye page yake ya Facebook alipost picha za walivyokamatwa navyo ‘Magaidi’ hawa.
Morogoro Maulid Kambaya June 27 2015
Morogoro 4
Morogoro 3
Morogoro 2Jiunge na mimi 

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI JUNE 27,2015



 

MAGAZETI YA LEO IJUMAA JUNE 26,2015 HAYA HAPA



     

    Big Sean ft. Kanye West, John Legend-One Man Can Change The World Download & Tazama HAPA

                                                          

    NATHANIEL CLYNE KUJIUNGA NA LIVERPOOL

     Nathaniel-Clyne-009
                                                                                                                                                          Nathaniel Clyne kujiunga Liverpool
    Nathaniel Clyne yuko mbioni kujiunga na Liverpool baada ya Klabu yake Southampton kuikubali Ofa ya Pauni Milioni 12.5.
    Clyne, ambae ni Fulbeki wa Kulia, anakuwa Mchezaji wa 6 kusainiwa na Liverpool katika kipindi hiki cha kuelekea Msimu mpya.
    Uhamisho huu wa Clyne, mwenye Miaka 24 na ambae ameichezea England mara 5, utakamilika baada ya upimaji wa Afya yake na makubaliano ya maslahi yake binafsi.
    Clyne atakuwa Mchezaji wa 4 kujiunga na Liverpool kutoka Southampton kufuatia wale waliojiunga Mwaka Jana ambao ni Adam Lallana, Dejan Lovren na Rickie Lambert.

    EVERTON YASAJIRI FORWARD WA BARCELONA

     
    Fowadi wa Barcelona Gerard Deulofeu 
    Everton wamemsaini Fowadi wa Barcelona Gerard Deulofeu kwa Dau la Pauni Milioni 4.3.
    Deulofeu, mwenye Miaka 21 na ambae ameichezea Spain mara 1, alikuwa na Everton kwa Mkopo Msimu wa 2013/14 na kisha kurejea Barcelona ambapo Msimu uliopita alipelekwa tena nje kwa Mkopo safari hii huko Sevilla.
    Mchezaji huyo ataanza kuwa Mchezaji rasmi wa Everton kuanzia Julai 1 na amesaini Mkataba wa Miaka Mitatu.
    Bosi wa Everton, Roberto Martinez, amesema anaamini  Deulofeu ana nafasi ya kukuwa na kuwa Mchezaji bora zaidi.
    Deulofeu anakuwa Mchezaji wa Pili kusainiwa na Everton katika kipindi hiki baada ya kumpata Kiungo wa England Tom Cleverley aliejiunga kama Mchezaji Huru baada ya Mkataba wake na Manchester United kumalizika kufuatia kuichezea Aston Villa kwa Mkopo Msimu uliopita.

    MRITHI WA DE GEA NJIANI KUTUA OLD TRAFFORD!!

    OLD-TRAFFORD                                                                                                                                                                         Zipo ripoti nzito toka England zinazodai Meneja wa Manchester United Louis van Gaal na Kipa wa Tottenham Hugo Lloris wamefikia muafaka na Kipa huyo wa Kimataifa wa France ambae ameshakubaliana kuhusu maslahi yake binafsi huko Old Trafford.
    Huku kukiwa na mipango ya chini chini ya Kipa Nambari Wani David de Gea kurudi kwao Spain kuidakia Real Madrid, kumchukua Hugo Lloris kunaelekea kuziba pengo hilo.
    Kwa mujibu wa chanzo cha habari hizi, Gazeti linaloheshimika huko France L'Equipe, kilichobaki sasa ni mazungumzo ya kukubaliana Ada ya Uhamisho na Mwenyekiti wa Tottenham Daniel Levy.
    L'Equipe imedai Levy amemhakikishia Lloris kuwa Klabu yeyote itakayotoa Ofa ya Pauni Milioni 18 kwenda juu basi atamruhusu kuhama White Hart Lane.
    Lloris, mwenye Miaka 28, alijiunga na Tottenham Mwaka 2012 akitokea Lyon ya France kwa Dau la Pauni Milioni 11.4.
    Hata hivyo, Levy anasifika mno kwa ugumu wa kutoa Wachezaji wake Nyota na kama akiwaruhusu basi Dau lao huwa sio masihara.

    VILABU VYATAKIWA KUWALIPIA KODI WALIMU NA WACHEZAJI

    UWANJA- TAIFA-DAR-1
     
    TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI - RELEASE NO. 105
    TAREHE 25 JUNI 2015
                                                                                                                                                                                                                     Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeviagiza vilabu vinavyoshiriki Ligi kuu ya nchini (mpira wa kulipwa) Tanzania, kuhakikisha kuwa wanalipa kodi kutokana na kuajiri makocha na wachezaji kutoka ndani na nje ya nchi.
    Kamshina wa TRA ameliagiza Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) kupitia kwa katibu mkuu wake kuwa, vilabu vyote vya mpira wa miguu nchini vinavyoajiri walimu, wachezaji kutoka ndani na nje ya nchi wahakikishe wanaweka kipengele cha kodi katika mikataba wanayoingia kuwaajiri.
    Vilbu vya vinapaswa kuwasilisha mikataba yote ya ajira ya wachezaji na walimu wao ili kukokotoa kodi stahiki kwa kila mmoja wao na mikataba yao kugongwa muhuri na stempu.
    Kwa mujibu wa sheria za Kodi ya Mapato ya mwaka 2004, kufungu namba 7, kila mtu anayepata mapato yatokanayo na ajira katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anawajibika kulipa kodi ya mapato kulingana na kipato chake.
    Aidha kwa mujibu wa Sheria ya Ushuru wa stempu ya mwaka 1973, kifungu namba 5 kikisomwa pamoja na jedwali la sheria hii, kila mkataba unatakiwa kugongwa muhuri na stempu na ofisa wa stempu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania.
    Kwa kuwa TFF ndio mlezi na msimamizi mkuu wa vilabu vya Mpira wa Miguu hapana nchini na hasa Ligi Kuu, tunaviomba vilabu vyote kuhakikisha vinawasilisha mikataba ya walimu na wachezaji yao ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa ajili ya kugongwa mihuri na stempu.
     
    Supported by AMAGA Media services : | |
    Copyright © 2015. UKURASA WA HABARI - All Rights Reserved
    Templete Designed by Abdallah Magana
    Proudly powered by Blogger