UEFA CHAMPIONZ LIGI
MAKUNDI
Jumanne Oktoba 20
**Mechi zote kuanza Saa 3 Dak 45 Usiku
KUNDI E
BATE Borislov v Barcelona
Bayer Leverkusen v AS Roma
KUNDI F
Arsenal v Bayern Munich
Dinamo Zagreb v Olympiakos
KUNDI G
Dynamo Kiev v Chelsea
FC Porto v Maccabi Tel Aviv
KUNDI H
Valencia v KAA Gent
Zenit Saint Petersburg v Lyon
++++++++++++++++++++++++++++++++++
JUMANNE Usiku Chelsea wapo huko Ukraine kucheza Mechi yao ya 3 ya Kundi G la UEFA CHAMPIONZ LIGI, UCL, na Dynamo Kiev lakini Meneja wao Jose Mourinho amekataa kuthibitisha kama Staa wao Eden Hazard atacheza Mechi hiyo.
Hazard alitupwa nje kwenye Mechi ya Jumamosi ya Ligi Kuu England walipoichapa Aston Villa 2-0 lakini Kikosi kilichosafiri kwenda huko Ukraine hakina Mastraika Pedro na Loic Remy ambao wamebakia London kutokana na maumivu.
Licha ya mapengo hayo, Mourinho amekataa kuthibitisha kama Hazard atacheza Mechi hii ya UCL ingawa ipo nafasi kubwa lazima atapata namba.
Mechi hii na Dynamo Kiev ni muhimu mno kwa Chelsea ambao kwenye Kundi G wapo Nafasi ya 3 baada ya kushinda Mechi 1 na kufungwa 1 wakiwa na Pointi 3 huku juu yao wapo Vinara Dynamo Kiev na FC Porto ambao wote wana Pointi 4 kila mmoja.
Mourinho mwenyewe amekiri hilo aliposema: “Tunahitaji kushinda Mechi. Hatufikirii wapi tulipo, inabidi tushinde Mechi inayotukabili.”
Dynamo, wakiwa kwao Kiev, si Timu ya ubwete ingawa Ijumaa iliyopita walikumbana na kipigo chao cha kwanza katika Mechi 38 za Ligi Kuu ya Ukraine baada kupigwa 3-0 na Shakhtar Donetsk lakini kwenye Mechi zao 10 zilizopita za Ulaya wameshinda 7 na kufungwa 1 tu.
UEFA CHAMPIONZ LIGI
MAKUNDI
Jumatano Oktoba 21
**Mechi zote kuanza Saa 3 Dak 45 Usiku
KUNDI A
Malmö FF v Shakhtar Donetsk
Paris St Germain v Real Madrid
KUNDI B
CSKA v Man United
VfL Wolfsburg v PSV
KUNDI C
Atletico Madrid v FC Astana
Galatasaray v Benfica
KUNDI D
Juventus v Borussia Mönchengladbach
Man City v Sevilla
0 comments:
Post a Comment