MENEJA
wa Chelsea Jose Mourinho atabakia kwenye kibarua chake kwa sasa licha
ya Jana kutandikwa 3-1 Uwanjani kwao Stamford Bridge na Liverpool kwenye
Mechi ya Ligi Kuu England ikiwa ni ni kipigo chao cha 6 katika Mechi 11 za Ligi hiyo Msimu huu.
Chelsea,
ambao ndio Mabingwa Watetezi wa Ligi Kuu England, wapo Nafasi ya 15
kwenye Msimamo wa Ligi wakiwa Pointi 14 nyuma ya Vinara Man City.
Akihojiwa
mara baada ya kipigo cha Jana kama anadhani hiyo ndio Mechi yake ya
mwisho kama Meneja, Mourinho alijibu: “Hapana. Sifikirii hilo!”
Mourinho,
ambae hajawahi kufungwa zaidi ya Mechi 6 za Ligi katika Msimu mmoja
akiwa kama Meneja wa Chelsea, aliongeza: “Mapambano yanaendelea lakini
wakati mwingine mapambano haya ni magumu kushinda. Unaingia kwenye
mapigano na silaha nyingine!”
MATOKEO:
Jumamosi Oktoba 31
Chelsea 1 Liverpool 1
Crystal Palace 0 Man United 0
Man City 2 Norwich 1
Newcastle 0 Stoke 0
Swansea 0 Arsenal 3
Watford 2 West Ham 0
West Brom 2 Leicester 3
RATIBA:
**Saa za Bongo
Jumapili Novemba 1
1630 Everton v Sunderland
1900 Southampton v Bournemouth
Jumatatu Novemba 2
2300 Tottenham v Aston Villa
Home »
» MOURINHO;KUBAKI CHELSEA LICHA VIPIGO MFULULIZO
0 comments:
Post a Comment