Zimebaki siku kumi kuifikia October 25
2015 siku ambayo Watanzania watafanya maamuzi ya kuchagua Viongozi wao
kwenye ngazi za Udiwani, Wabunge pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano…
stori zinazohusu Siasa ziko pia kwenye Headlines kila siku.
October 15 2015 baadhi ya Viongozi wa CHADEMA wamekaa Kikao na kujadili masuala makubwa mawili kuelekea siku ya Uchaguzi Mkuu 2015.
Kwanza ni hii kuhusu umbali ambao watu wanatakiwa kukaa baada ya kupiga kura >>> “Baada
ya Wananchi kupiga kura, wasogee mita 200 wakae kulinda kura zao… Sio
jambo la Kijinai,Sheria inaruhusu hivyo. Viongozi wanaoondoka Madarakani
hawajui chochote kuhusiana na Sheria ya Uchaguzi” >>> John Mallya.
“Hivi
Vituo vya Kupiga Kura haviko Mbinguni, kama ni Shule au Ofisi ya Kata
ziko sehemu ya Makazi ya watu, sasa hao watu utawaambia nyumbani kwao
waondoke siku hiyo?” >>> Hiki ndio alichokisema Mwanasheria wa CHADEMA, John Mallya.
Lakini kingine ilikuwa ni ishu ya Daftari la Wapigakura >>>> “Tumekuwa
tukiiomba Tume ya Uchaguzi itoe Daftari, baada ya kushinikiza sana
wametupa Daftari jana jioni.. Tumekuta matatizo baada ya kulipitia
Daftari, katika Kituo kimoja tu kuna makosa zaidi ya 17.. ndani ya
Daftari kuna Wachina wameandikishwa, kuna Godown, pikipiki vyote
vimepigwa picha na kupewa Kadi za Kupigia Kura… Imekuwaje Tume
imeshindwa kugundua tatizo hili, kwenye Picha nyingine za Vitambulisho
watu wamejipiga selfie” >>> Reginald Munisi, Mkurugenzi Uchaguzi CHADEMA.
Hapa ni Pichaz zinazoonesha baadhi ya makosa ambayo wameyagundua kwenye Daftari la Wapigakura.
credit na Millardayo.com
0 comments:
Post a Comment