Kagame kuiongoza Rwanda hadi 2034?


 

 Bunge la Rwanda limepitisha sheria itakayomruhusu rais Paul Kagame kugombea tena urais kwa mihula miwili. Muhula wa kwanza utakuwa wa miaka saba na unaofuata wa miaka mitano.
Hii kutangazwa kwa uamuzi huu umehitimisha safari ya miezi mitatu iliyoanza mwezi wa saba ambapo bunge la Rwanda lilianza mchakato mchakato wa mabadiliko ya katiba. Akizungumza bungeni baada ya kupitisha uamuzi huo, spika wa bunge la Rwanda Donatille Mukabarisa amesema: "Tumeweka muhula wa miaka saba pekee ambayo unafuata muhula huu unaomalizika na unaozungumziwa kwenye kipengele kilichotangulia. Tumeuweka muhula huu kama wa mpito tu kwa sababu kwa mujibu wa sheria kunapotokea mabadiliko ni lazima kuwepo na kipindi cha kuweka mambo sawa, na hii ni kwa sababu tunataka kuelekea kule tunakopenda."
Katiba ya Rwanda kulingana na nchi za Afrika Mashariki
Uamuzi huo umeridhiwa na wabunge wote 80 wa wabunge la Rwanda lakini mjadala uliochukua muda ni ule kuhusu baadhi ya vipengele vingine hasa kile kinachohusu hatima ya Rais anapostaafu. "Ni lazima tutazame pia mahitaji zaidi kwa rais anayeomba kuwa seneta baada ya kumaliza muhula wake kwa sababu kuwahi kuwa Rais hakupaswi kumpa mtu tiketi ya moja kwa moja ya Rais na hii ni kwa sababu anaweza kuwa alifanya mambo ambayo hayawezi kumruhusu kufanya kazi hiyo ya useneta," amesema mbunge mmoja.
Mabadiliko haya ya katiba yanakwenda mbali na kusema kwamba baada ya muhula huo wa miaka saba Rwanda itaendelea na mihula ya miaka mitano inayompa Rais nafasi kugombea mara mbili tu. Lakini la miaka saba na miaka mitano likaonekana kwuachanganya baadhi ya wananchi.
Spika wa bunge amesema kimsingi wabunge wamepitisha uamuzi huo ili kwamba baadaye katiba ya Rwanda iende sambamba na nchi nyingine za Jumuiya ya Afrika Mashariki hasa kuhusu mihula ya miaka 5 ya urais. Kutokana na mabadiliko haya huenda sasa Rais Paul Kagame akaitawala Rwanda hadi mwaka 2034.

MOURINHO;KUBAKI CHELSEA LICHA VIPIGO MFULULIZO

 MOURINHO-SHINGONI                                                                                                                                    MENEJA wa Chelsea Jose Mourinho atabakia kwenye kibarua chake kwa sasa licha ya Jana kutandikwa 3-1 Uwanjani kwao Stamford Bridge na Liverpool kwenye Mechi ya Ligi Kuu England ikiwa ni ni kipigo chao cha 6 katika Mechi 11 za Ligi hiyo Msimu huu.
Chelsea, ambao ndio Mabingwa Watetezi wa Ligi Kuu England, wapo Nafasi ya 15 kwenye Msimamo wa Ligi wakiwa Pointi 14 nyuma ya Vinara Man City.
Akihojiwa mara baada ya kipigo cha Jana kama anadhani hiyo ndio Mechi yake ya mwisho kama Meneja, Mourinho alijibu: “Hapana. Sifikirii hilo!”
Mourinho, ambae hajawahi kufungwa zaidi ya Mechi 6 za Ligi katika Msimu mmoja akiwa kama Meneja wa Chelsea, aliongeza: “Mapambano yanaendelea lakini wakati mwingine mapambano haya ni magumu kushinda. Unaingia kwenye mapigano na silaha nyingine!”
MATOKEO:
Jumamosi Oktoba 31
Chelsea 1 Liverpool 1       
Crystal Palace 0 Man United 0              
Man City 2 Norwich 1                
Newcastle 0 Stoke 0                  
Swansea 0 Arsenal 3        
Watford 2 West Ham 0               
West Brom 2 Leicester 3   
RATIBA:
**Saa za Bongo
Jumapili Novemba 1
1630 Everton v Sunderland                  
1900 Southampton v Bournemouth                 
Jumatatu Novemba 2
2300 Tottenham v Aston Villa
 BPL-STAND-OCT31

SAMATTA AIPA USHINDI TP MAZEMBE KLABU BINGWA AFRIKA-FAINALI

MAZEMBE                                                                                                                                STRAIKA mahiri wa Tanzania Mbwana Samatta Jana Usiku alifunga Bao la ushindi kwa Klabu yake TP Mazembe ya Congo DR walipocheza Mechi ya Kwanza ya Fainali ya CAF CHAMPIONZ LIGI dihidi ya USM d’Alger huko Algiers na kushinda 2-1.
Bao hilo la Samatta lilifungwa kwa Penati katika ya Dakika ya 79.
TP Mazembe walitangulia kufunga Bao katika Dakika ya 27 kupitia Rainford Kalaba na Mchezaji huyo kutolewa kwa Kadi Nyekundu Dakika ya 45.
Nao USM d’Alger walibaki Mtu 10 kuanzia Dakika ya 67 baada ya Hocine El Orfi kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu na Mazembe kupewa Penati ambayo Nathan Sinkala wa Zambia alikosa.
USM d’Alger walisawazisha katika Dakika ya 88 kwa Bao la Mohamed Sequer lakini Mtanzania Mbwana Samatta akaleta ushindi kwa Bao lake la Penati na TP Mazembe kuibuka kidedea kwa Bao 2-1.
Marudiano ya Fainali hii ni Novemba 8 huko Lubumbashi, Congo DR.
Mshindi wa Fainali hizi atazoa Donge la Dola Milioni 1.5 na pia ataiwakilisha Afrika kwenye Mashindano ya FIFA ya Klabu Bingwa Duniani huko Japan Mwezi Desemba.
CAF CHAMPIONZ LIGI
FAINALI
Ratiba/Matokeo:
**Saa za Bongo
Jumamosi Oktoba 31
Union Sportive Medina d’Alger [Algeria] 1 TP Mazembe [Congo, DR] 2
Marudiano
Jumapili Novemba 8
1630 TP Mazembe v Union Sportive Medina d’Alger

Kauli ya kwanza ya Dr. Magufuli baada ya ushindi wa urais na shangwe za ...

 
Baada ya Rais mteule wa Tanzania, Dr. John Magufuli na Makamu wake Mama Samia Suluhu Hassan kukabidhiwa cheti na Tume ya Uchaguzi NEC, safari ilianza toka Ukumbi wa Diamond Jubilee Upanga mpaka Ofisi za CCM mtaa wa Lumumba Dar ambapo wanaCCM na viongozi wengine walikusanyika.
Video yake kwenye kile alichokisema kwenye Jukwaa la CCM mtaa wa Lumumba hiki hapa…

                                                         

CONGRATULATION MY LOVE BROTHER.....

UEFA CHAMPIONS LEO; DYNAMO Vs CHELSEA: MOURINHO HAZARD KUCHEZA, PEDRO, REMY WABAKI LONDON!

MOURINHO-MIMACHO


                                                                                                                                       UEFA CHAMPIONZ LIGI
MAKUNDI
Jumanne Oktoba 20
**Mechi zote kuanza Saa 3 Dak 45 Usiku
KUNDI E
BATE Borislov v Barcelona          
Bayer Leverkusen v AS Roma                
KUNDI F
Arsenal v Bayern Munich             
Dinamo Zagreb v Olympiakos               
KUNDI G
Dynamo Kiev v Chelsea              
FC Porto v Maccabi Tel Aviv                  
KUNDI H
Valencia v KAA Gent         
Zenit Saint Petersburg v Lyon
++++++++++++++++++++++++++++++++++
JUMANNE Usiku Chelsea wapo huko Ukraine kucheza Mechi yao ya 3 ya Kundi G la UEFA CHAMPIONZ LIGI, UCL, na Dynamo Kiev lakini Meneja wao Jose Mourinho amekataa kuthibitisha kama Staa wao Eden Hazard atacheza Mechi hiyo.
Hazard alitupwa nje kwenye Mechi ya Jumamosi ya Ligi Kuu England walipoichapa Aston Villa 2-0 lakini Kikosi kilichosafiri kwenda huko Ukraine hakina Mastraika Pedro na Loic Remy ambao wamebakia London kutokana na maumivu.
Licha ya mapengo hayo, Mourinho amekataa kuthibitisha kama Hazard atacheza Mechi hii ya UCL ingawa ipo nafasi kubwa lazima atapata namba.
Mechi hii na Dynamo Kiev ni muhimu mno kwa Chelsea ambao kwenye Kundi G wapo Nafasi ya 3 baada ya kushinda Mechi 1 na kufungwa 1 wakiwa na Pointi 3 huku juu yao wapo Vinara Dynamo Kiev na FC Porto ambao wote wana Pointi 4 kila mmoja.
Mourinho mwenyewe amekiri hilo aliposema: “Tunahitaji kushinda Mechi. Hatufikirii wapi tulipo, inabidi tushinde Mechi inayotukabili.”
Dynamo, wakiwa kwao Kiev, si Timu ya ubwete ingawa Ijumaa iliyopita walikumbana na kipigo chao cha kwanza katika Mechi 38 za Ligi Kuu ya Ukraine baada kupigwa 3-0 na Shakhtar Donetsk lakini kwenye Mechi zao 10 zilizopita za Ulaya wameshinda 7 na kufungwa 1 tu.
UCL-G
UEFA CHAMPIONZ LIGI
MAKUNDI
Jumatano Oktoba 21
**Mechi zote kuanza Saa 3 Dak 45 Usiku
KUNDI A
Malmö FF v Shakhtar Donetsk              
Paris St Germain v Real Madrid             
KUNDI B
CSKA v Man United          
VfL Wolfsburg v PSV                  
KUNDI C
Atletico Madrid v FC Astana                 
Galatasaray v Benfica                 
KUNDI D
Juventus v Borussia Mönchengladbach             
Man City v Sevilla            

Magazeti ya Tanzania leo October 20, 2015

 
.
.

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
 
Supported by AMAGA Media services : | |
Copyright © 2015. UKURASA WA HABARI - All Rights Reserved
Templete Designed by Abdallah Magana
Proudly powered by Blogger