YANGA WAINGIA JIJINI MBEYA KWA MBWEMBWE
Kikosi cha Yanga SC kimeingia jioni ya leo jijini mbeya kwa mchezo wa Ligi kuu Tanzania bara Dhidi ya Wenyeji wao Wana Jela jela Tanzania Prisons timu ambayo inamilikiwa na Jeshi la Magereza.

Mchezo huo ambao utachezwa siku ya Alhamis katika Dimba la Sokoine Jijini Mbeya Unatarajiwa kuwa mgumu kutokana na Ugumu wa ligi hiyo kwani Prisons wakifungwa wanakua katika mazingira mabaya ya kushuka Daraja huku Mabingwa wa zamani Wa Tanzania Bara Yanga wakifanya juhudi za kurudisha ubingwa wao waliopokonywa na Azam Fc msimu uliopita.
Yanga Sc itashuka Dimbani tena siku ya jumapili katika Uwanja huo huo wa Sokoine Jiji Mbeya na Watakua na Kazi ngumu dhidi ya wana Amsha Amsha,Wabishi wa Ligi Mbeya City Council SC Ikiwa ni mchezo wa kipolo wa Round ya kwanza ya Ligi kuu Tanzania bara
SHULE ZA SECONDARY ZA BINAFSI ZAONGOZA 10 BORA KIDATOCHA NNE
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani nchini,Dk. Charles Msonde akizungumza na wanahabari jijini Dar leo.
Shule za sekondari za binafsi zaongoza 10 bora matokeo ya mtihani wa kidato cha nne uliofanyika mwaka jana.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam, Katibu
Mtendaji wa Baraza la Mitihani nchini (NECTA), Dk.Charles Msonde
amesema katika matokeo ya kidato cha nne ya mtihani wa mwaka jana ufaulu
umeongezeka kwa asilimia 12.67 ikilinganishwa na mwaka 2013.
Katika matokeo hayo msichana wa shule ya sekondari ya Baobab, Nyakaho I. Marungu ndio aliyeongoza mtihani huo na kufatia…
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani nchini,Dk. Charles Msonde akizungumza na wanahabari jijini Dar leo.
Shule za sekondari za binafsi zaongoza 10 bora matokeo ya mtihani wa kidato cha nne uliofanyika mwaka jana.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam, Katibu
Mtendaji wa Baraza la Mitihani nchini (NECTA), Dk.Charles Msonde
amesema katika matokeo ya kidato cha nne ya mtihani wa mwaka jana ufaulu
umeongezeka kwa asilimia 12.67 ikilinganishwa na mwaka 2013.(P.T)
Katika
matokeo hayo msichana wa shule ya sekondari ya Baobab, Nyakaho I.
Marungu ndio aliyeongoza mtihani huo na kufatia wavulana.
Shule za
Sekondari za St.Fransis ya mkoani Mbeya wanafunzi sita na Feza wanafunzi
nane na kufanya shule hizo kuingia katika 10 bora kwa kutoa idadi
wanafunzi wengi ikilinganishwa na shule zingine.
Msonde amasema matokeo hayo yanatokana na mfumo mpya wa GPA kwa kuangalia masomo saba hivyo ufaulu umetokana na mfumo huo.
BOFYA LINK HII KUONA NA KUSOMA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE NA QT 2014 .
KUANGALIA MATOKEO BONYEZA HAPA =====> MATOKEO KIDATO CHA NNE 2014