Home » » YANGA WAINGIA JIJINI MBEYA KWA MBWEMBWE

YANGA WAINGIA JIJINI MBEYA KWA MBWEMBWE



                   
Kikosi cha Yanga SC kimeingia jioni ya leo jijini mbeya kwa mchezo wa Ligi kuu Tanzania bara Dhidi ya Wenyeji wao Wana Jela jela Tanzania Prisons timu ambayo inamilikiwa na Jeshi la Magereza.
 



Mchezo huo ambao utachezwa siku ya Alhamis katika Dimba la Sokoine Jijini Mbeya Unatarajiwa kuwa mgumu kutokana na Ugumu wa ligi hiyo kwani Prisons wakifungwa wanakua katika mazingira mabaya ya kushuka Daraja huku Mabingwa wa zamani Wa Tanzania Bara Yanga wakifanya juhudi za kurudisha ubingwa wao waliopokonywa na Azam Fc msimu uliopita.

     

Yanga Sc itashuka Dimbani tena siku ya jumapili katika Uwanja huo huo wa Sokoine Jiji Mbeya na Watakua na Kazi ngumu dhidi ya wana Amsha Amsha,Wabishi wa Ligi Mbeya City Council SC Ikiwa ni mchezo wa kipolo wa Round ya kwanza ya Ligi kuu Tanzania bara                        

Toa maoni yako kwa habari hii kwa kuweka email yako hapa,na endelea kutufatilia zaidi Ukurasa wa habari

0 comments:

 
Supported by AMAGA Media services : | |
Copyright © 2015. UKURASA WA HABARI - All Rights Reserved
Templete Designed by Abdallah Magana
Proudly powered by Blogger