TANZANIA YANG'ARA TENA.....IDRIS SULTAN ASHINDA BIG BROTHER AFRICA HOTSHOTS 2014

Leo ni siku ya 63 tangu yaanze mashindano ya Big Brother Africa, ndiyo siku ambayo imefanyika fainali ya #BBAHotshots kwa mwaka huu 2014.

Labda nikukumbushe kwamba Tanzania ndiyo nchi pekee iliyokuwa imebakiwa na mshiriki wake ndani ya Jumba la BBA katika ukanda wa Afrika Mashariki na tuliona namna ambavyo mastaa wengi wakitoa support kubwa kwa mshiriki huyo ambaye ni Idris.

Hatimaye usiku huu wa Desemba 07 historia nyingine imeandikwa Afrika, ambapo mwakilishi huyo kafanikiwa kuibuka mshindi.

Nimepita katika kurasa za mastaa mbalimbali Twitter, hiki ndicho kilichoandikwa na mastaa hao;
YEEEES!!! FINALLY !!! $300,000 cash prize for @BigBroAfrica #BBAHotShots comes to East Africa ! Congratulations to our bro @IdrisSultan !!!

DIAMOND HATUA WASHINGTON DC
Diamond akiwasili kwenye uwanja wa kimataifa wa Dulles muda huu tayari kwa makamuzi ya sharehe ya Uhuru itayofanyika muda si mrefu Sheraton, ya Downtown Silver Spring, Maryland.
Diamond akimsalimia mwenyeji wake hayupo pichani mara tu alipowasili Dulles.
Kutoka kushoto ni Dj Romy Jones, Diamond na mmoja wa waratibu wa sherehe ya Uhuru Bwn. Phanuel Ligate.
