ERASTO NYONI AJIFUNGA MIAKA MIWILI SIMBA

'Beki Erasto Nyoni asaini mkataba wa miaka miwili kuichezea klabu ya Simba akitokea Azam FC https://www.djboytz.com'
  •  Beki/kiungo Erasto Nyoni asaini kandarasi ya miaka miwili kuichezea klabu ya Simba. akitokea katika Azam FC.
Image may contain: 4 people

FULL VIDEO; Tundu Lissu alivyogoma kutoka Mahakamani ili asikamatwe na Polisi Dodoma

 









July 19, 2017 Mbunge wa Singida mashariki Tundu Lissu
aligoma kutoka katika chumba cha Mahakama ya wilaya Dodoma alipokuwa
akifanya shughuli zake za uwakili kwa kuhofia kukamatwa na Polisi
waliosemekana kumsubiri nje wamkamate kwa tuhuma za uchochezi.


Akiwa ndani ya Mahakama, Tundu Lissu aliongea mbele
ya Waandishi wa habari Dodoma na kusema kuwa alibaini njama za Polisi
kutaka kumkamata baada ya kupata taarifa kutoka kwa Mke wake  na kwamba
Polisi walianzia kumtafuta nyumbani Dar es salaam kabla ya kufahamu kuwa
yuko Dodoma.


Kwenye hii video hapa chini Tundu Lissu anaonekana akielezea mkasa huo…

MAGAZETI YA LEO JULY 20,2017 HAYA HAPA

 

BREAKING: Mama mzazi wa mpenzi wa Diamond, Zari the boss amefariki

Mama mzazi wa Zari The Boss Lady ambaye ni mpenzi na mzazi mwenza wa mwimbaji wa Bongofleva Diamond Platnumz amefariki dunia asubuhi hii baada ya kuumwa.
Kupitia Instagram yake asubuhi hii Zari amethibitisha kifo cha mama yake.
Zari ameandika>>>”It’s with deep sorrow that my family and I announce the death of our lovely mother who passed on this morning. May her soul rest in peace, May Allah forgive you your sins and grant you Jana. You will forever be loved our Old Sun, us as your kids were given the best from God as our mother. We appreciate all you did for us. We will forever cherish you Mama. Sleep well😢

DTB YAMWAGA MAMILIONI TFF

 
BENKI ya Diamond Trust Bank DTB imesaini mkataba na Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) wenye thamani ya sh 250 milioni kwa ajili ya kudhamini ligi kuu ya Vodacom kwa mwaka mmoja.

Akizungumza kwenye hafla ya utiaji saini uliofanyika kwenye Hotel ya Serena Mkuu wa kitengo cha Fedha wa Benki hiyo Joseph Mabusi alisema udhamini huo utasaidia maendeleo ya soka nchini kwa kuziwezesha timu shiriki kujiandaa vya kutosha ili kuwa na ligi bora yenye ushindani wa kweli.

"Tunafurahi na kujivunia kuwa sehemu ya soka tunawaahidi wadau wa soka kuendelea kuwa pamoja nao kwa muda mwingi zaidi licha ya kusaini mwaka mmoja,"alisema Mabusi.

Kwa upande wake Rais wa TFF Jamal Malinzi ameishukuru benki hiyo kujitokeza kudhamini ligi huku akitanabaisha kuwa udhamini huo umefika muda muafaka kutokana na Shirikisho kuandamwa na mambo mengi yanayohitaji fedha.

"Ninawashukuru DTB kwa kujitokeza kudhamini, na pia nichukue nafasi hii kuyakaribisha makampuni mengine kuendelea kujitokeza ili tuweze kuwa ligi bora," alisema Malinzi.

Nae Mwenyekiti wa bodi ya ligi Hamadi Yahaya ameitoa hofu Benki hiyo kuwa pesa zilizotolewa zitaenda kutumika kwa malengo yaliyokusudiwa huku wakijiandaa kukaa na timu shiriki ili kuangalia jinsi ya kuzigawa.

Wakati huo huo Mwakilishi wa klabu ambaye ni Mwenyekiti wa African Lyon Rahim Zamunda alisema kuwa ili taifa liweze kufika mbali katika medani ya soka lazima uwekezaji mkubwa uendelee kufanywa na makampuni mbali mbali kwakua mpira ni ajira kwa sasa.
 
Supported by AMAGA Media services : | |
Copyright © 2015. UKURASA WA HABARI - All Rights Reserved
Templete Designed by Abdallah Magana
Proudly powered by Blogger