MAGAZETI YA LEO DECEMBER 4,2014 YAPO HAPA





   
.   .
.
.

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

MAKUNDI YA AFCON 2015 YAPO HAPA

  africacupofnations_shkzvwhv6ezr1s48is3xs2ekk
Timu 16 zilizofuzu kushiriki michuano ya kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2015 huko Equatorial Guinea zimepangwa katika makundi manne usiku huu katika hafla ya upangaji makundi iliyofanyika jijini Malabo ambako fainali hizo zitafanyika .
Makundi hayo yanaonyesha kuwa timu mwenyeji Equatorial Guinea imepangwa kwenye kundi ambako itakuwa na timu za Burkina Faso , Gabon pamoja na Congo brazzavile .
Timu namba moja barani Afrika ya Algeria imepangwa Kundi C na timu za Afrika Kusini , Senegal na Ghana.
Timu namba moja barani Afrika ya Algeria imepangwa Kundi C na timu za Afrika Kusini , Senegal na Ghana.
Kundi B limejumuisha timu za Zambia , Tunisia , Cape Verde na Congo Drc , .
Kundi jingine ambalo ni kundi C lina timu za Ghana , Afrika Kusini, Senegal na Algeria huku Kundi D likiwa na timu za Ivory Coast, Guinea , Cameroon na Mali .
Mabingwa wa Afcon 2013 Nigeria hawataweza kutetea ubingwa wao baada ya kushindwa kufuzu.
Mabingwa wa Afcon 2013 Nigeria hawataweza kutetea ubingwa wao baada ya kushindwa kufuzu.
Michuano hiyo ambayo awali ilikuwa ifanyike nchini Morocco kabla ya kuhamishiwa nchini Equatorial Guinea itafanyika kati ya Januari 15 na Februari 8 mwakani.
Kundi A .
Equatorial Guinea
Gabon
Burkina Faso
Congo Brazzaville.

Kundi B
Zambia
Tunisia
Cape Verde
Congo Drc

Kundi C
Ghana
Afrika Kusini
Senegal
Algeria

Kundi D.
Ivory Coast
Cameroon
Guinea.
Mali.
Michuano hii itafanyika kwenye miji minne huko Equatorial Guinea ambako Kundi A litacheza mechi zake kwenye kituo cha kwanza ambacho kiko kwenye mji wa Bata , Kundi B litakuwa litakuwa huko Ebibeyin , Kundi C litachezea kwenye mji wa Mongomo na Kundi litakuwa kwenye mji mkuu wa Equatorial Guinea huko Malabo.

RASHID MANDAWA MCHEZAJI BORA LIGI KUU TANZANIA BARA

 

MANDAWA (KUSHOTO) AKIWA NA WACHEZAJI WENZAKE WA KAGERA SUGAR
Mshambuliaji wa timu ya Kagera Sugar, Rashid Mandawa ya mkoani Kagera amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kwa mwezi Novemba mwaka huu ambapo atazawadiwa kitita cha sh. milioni moja.

Mandawa ambaye kwa mwezi huo alichuana kwa karibu na mshambuliaji Fulgence Maganda wa Mgambo Shooting ya Tanga na nahodha wa Simba, Joseph Owino atakabidhiwa zawadi yake na wadhamini wa ligi hiyo kampuni ya Vodacom.
Hafla ya kukabidhi zawadi hiyo inatarajiwa kufanyika wakati wa mechi ya raundi ya nane ya ligi hiyo kati ya Simba na Kagera Sugar itakayochezwa Desemba 26 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
 
Chanzo Saleh Jembe

ALSHABAAB WAKARI KUWAUA WAKENYA 36



Kundi la wanamgambo nchini Somalia Al Shabaab limekiri kuwaua watu 36 katika shambulio lililotokea kwenye machimbo ya kokoto karibu na mji wa Mandera kaskazini mwa Kenya.

Katika taarifa iliyotolewa kwenye mtandao wa kundi hilo, wanamgambo hao wamesisitiza kuwa ndio waliowaua wakenya hao kwa sababu ya majeshi ya Kenya kuendelea kuwa nchini Somalia.
Taarifa za mauaji hayo zilitolewa kwa mara ya kwanza na Shirika la Msalaba Mwekundu.

Wakazi wa eneo hilo wamesema waathirika wote wa tukio hilo ni watu wasio Waislam ambao walikuwa wakifanya kazi katika machimbo hayo yaliyopo Kormey kilomita 15 kutoka mji wa Mandera Kaskazini mwa Kenya.

Tukio hili linafuatia tukio la wiki moja iliyopita ambapo watu wapatao 28 waliuawa katika shambulio la basi la abiria huko Mandera.



 
Watu wengine 26 waliuawa na wapiganaji hao mjini Mandera wiki iliyopita

Kundi la wapiganaji wa Kiislam la Al Shabab wamekiri kuhusika na mauaji hayo.
Mkuu wa Polisi hilo amesema bado wanafuatilia tukio hilo.

Katika tukio lingine, mtu mmoja ameripotiwa kuuawa nchini Kenya kufuatia mlipuko katika klabu moja ya usiku katika mji wa Wajir kaskazini mwa Kenya.

 Basi walimokuwa wakisafiria wakenya wengine waliouawa na Al Shabaab mjini Mandera wiki iliyopita

Kwa mujibu wa Kamishna wa Polisi wa Wajir, Frederick Sishia, shambulio hilo limefanyika saa mbili usiku na kuua mtu mmoja na watu wengine wanne wamejeruhiwa.

Washambuliaji hao walitumia magruneti na silaha nyingine za kijeshi kufanya shambulio hilo.
Wiki iliyopita watu wengi waliuawa eneo la Mandera kaskazini mwa Kenya.

Kenya imejikuta ikilengwa na mashambulio ya kigaidi tangu majeshi yake yapelekwe nchini Somalia kukabiliana na wapiganaji wa Al Shabab. Mbali na miji ya kaskazini mwa Kenya kushambuliwa kila mara, miji mikubwa nchini humo ya Nairobi na Mombasa imekuwa ikilengwa na mashambulio ya kigaidi.

Chanzo.bbc

YACINE BRAHIMI MCHEZAJI BORA AFRIKA 2014




yacine


Kituo cha habari cha Uingereza  BBC kimemtaja nyota wa timu ya taifa ya Algeria Yacine Brahimi kuwa mchezaji bora wa Afrika kwa mwaka 2014.

Brahimi ambaye anachezea klabu ya Ureno ya Fc Porto anakuwa raia wa kwanza wa Algeria kutwaa tuzo hiyo ambayo hutolewa na BBC kila mwaka .

Yacine Brahimi ametwaa tuzo ya BBC ya mchezaji bora wa Afrika .
 Yacine Brahimi ametwaa tuzo ya BBC ya mchezaji bora wa Afrika .

Brahimi ametwaa tuzo hii kufuatia uwezo aliouonyesha kwa mwaka huu akiwa na timu yake ya taifa hasa kwenye michuano ya kombe la dunia ambako Algeria walifanikiwa kufika hatua ya 16 bora .

BBC imekuwa na utaratibu wa kuandaa tuzo hizi kila mwaka ambapo kwa miaka miwili iliyopita kiungo wa Ivory Coast Yaya Toure amekuwa akitawala .
 
 FBL-WC-2014-MATCH54-GER-ALG

NJOMBE YAONGOZA KWA TAKWIMU ZA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI TANZANIA



 Katika kuazimisha siku ya kupiga vita  Ukimwi duniani wizara ya afya nchini Tanzania imetoa Takwimu za maambukizi ya ukimwi kwa mikoa ambapo mkoa wa Njombe umeongoza kwa maambukizi hayo



 
Supported by AMAGA Media services : | |
Copyright © 2015. UKURASA WA HABARI - All Rights Reserved
Templete Designed by Abdallah Magana
Proudly powered by Blogger