Taarifa
kutoka katikati ya Jiji Dar es Salaam, hali haikuwa shwari leo asubuhi,
tukio kubwa ni ajali ya moto ambao ulianza katika majengo
yanayomilikiwa na Shirika la Nyumba NHC.
Moto ulianza saa tatu asubuhi mtaa wa
Libya na Mosque, ambapo ulishika katika majengo matatu ya ghorofa
yaliyoongozana na kuunguza vitu ambavyo thamani yake haijafamika.
Vikosi vya Zimamoto vilifika na kuudhibiti moto huo huku wakiendelea na uchunguzi kujua chanzo cha moto huo.
Kamanda wa Polisi Suleiman Kova amesema hakuna mtu aliyefariki wala kuumia kutokana na ajali hiyo.
Hapa kuna picha za tukio hilo.
Pichaz zote nimezitoa: Issamichuzi.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment