RAIS KIKWETE ATEUA WAKUU WA WILAYA WAPYA 27
RAIS
Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko ya Wakuu wa Wilaya kwa kuwateua Wakuu
wapya 27, kuwahamisha vituo vya kazi 64 na wengine 42 amewabakisha
kwenye vituo vyao vya kazi vya zamani.
Akizungumza
na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa OWM TAMISEMI leo mchana
(Jumatano, Februari 18, 2015) Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema
mabadiliko hayo yamesababishwa na kuwepo kwa nafasi wazi 27 ambazo
zilitokana na wakuu wa wilaya watatu kufariki dunia; kupandishwa cheo
wakuu wa wilaya watano, kupangiwa majukumu mengine wakuu wa wilaya saba
na kutenguliwa kwa uteuzi wa wakuu wa wilaya 12.
Hata
hivyo, Waziri Mkuu alisema, Rais Kikwete amewabadilisha vituo vya kazi
wakuu wa wilaya 64 na kuwabakiza kwenye vituo vyao vya zamani wakuu wa
wilaya 42.
Wakuu wa
Wilaya wapya 27 walioteuliwa ni Mariam Ramadhani Mtima anayeenda
Ruangwa; Dk. Jasmine B. Tiisike anayeenda Mpwapwa; Pololeti Mgema
(Nachingwea); Fadhili Nkurlu anayeenda Misenyi; Felix Jackson Lyaniva
anayeenda Rorya na Fredrick Wilfred Mwakalebela anayeenda wilayaya
Wanging'ombe.
Wengine
na vituo vyao kwenye mabano ni Zainab Rajab Mbussi (Rungwe); Francis K.
Mwonga (Bahi); Kanali Kimiang'ombe Samwel Nzoka (Kiteto), Husna Rajab
Msangi (Handeni), Emmanuel J. Uhaula (Tandahimba); Mboni Mhita
(Mufindi); Hashim S. Mgandilwa (Ngorongoro); Mariam M. Juma (Lushoto);
Thea Medard Ntara (Kyela); Ahmad H. Nammohe (Mbozi); Shaban Kissu
(Kondoa) na Stephen Zelothe (Musoma).
Wengine
ni Pili Moshi (Kwimba); Mahmoud A. Kambona (Simanjiro); Glorius B. Luoga
(Tarime); Zainab R. Telack (Sengerema); Bernard Nduta (Masasi); Zuhura
Mustafa Ally (Uyui); Paulo Makonda (Kinondoni); Mwajuma Nyiruka
(Misungwi) na na Maftah Ally Mohamed (Serengeti).
Wakuu wa
Wilaya saba ambao uteuzi wao umetenguliwa lakini watapangiwa kazi
nyingine ni Brig. Jenerali Cosmas Kayombo aliyekuwa Simanjiro; Kanali
Ngemela E. Lubinga (aliyekuwa Mlele); Juma S. Madaha (aliyekuwa Ludewa);
Mercy E. Silla (aliyekuwa Mkuranga); Ahmed R. Kipozi (aliyekuwa
Bagamoyo); Mrisho Gambo (aliyekuwa Korogwe) na Elinas A. Pallangyo
(aliyekuwa Rombo).
Waziri
Mkuu pia aliwataja Wakuu wa Wilaya 12 ambao uteuzi wao umetenguliwa
kutokana na sababu za umri, kiafya na kuimarisha utendaji Serikaini na
wilaya zao kwenye mabano kuwa ni James K. Ole Millya (Longido); Elias
Wawa Lali (Ngorongoro); Alfred Ernest Msovella (Kongwa); Danhi Beatus
Makanga (Kasulu); Fatma Losindilo Kimario (Kisarawe); Elibariki E. Kingu
(Igunga); Dk. Leticia Moses Warioba (Iringa); Evarista N. Kalalu
(Mufindi); Abihudi M. Saideya (Momba); Martha J. Umbulla (Kiteto);
Khalid J. Mandia (Babati) na Elias Goroi (Rorya).
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
DODOMA. FEBRUARI 18, 2015.
MANCHERSTER UNITED YATINGA ROBO FAINALI YA FA CUP,,USO KWA USO NA ARSENAL
Manchester United umetinga robo fainali ya kombe la FA baada ya kuifunga Preston Noth End magoli 3-1 katika uwanja wa Old Trafford,Wageni walikuwa wakwanza kupata goli katika Dk 47 kupitia kwa Scott Laird alipiga shuti kali ambalo lilimbabatiza kipa David De Gea na kutinga Nyavuni.
Lakini Mashetani wekundu Man Utd wakazawasha Dakika ya 65 Baada ya Ander Herrera kupiga shuti na ambalo liliwapita mabeki pamoja na kipa wa Preston,Dakika ya 72 Marouane Fellaine akaipatia Man Utd goli la pili kabla ya Kaptain Wayne Rooney kufunga Goli la 3 katika Dakika za lala salama kwa mkwaju wa penati. Mpaka dakika 90 zinakamilika Man Utd 3-1 Preston Noth End.
Kwa matokeo hayo Manchester United Wametinga robo fainali ya kombe hilo Ambapo watakutana na Arsenal Machi 7 au 8 katika Uwanja wa Old Trafford.
Lakini Mashetani wekundu Man Utd wakazawasha Dakika ya 65 Baada ya Ander Herrera kupiga shuti na ambalo liliwapita mabeki pamoja na kipa wa Preston,Dakika ya 72 Marouane Fellaine akaipatia Man Utd goli la pili kabla ya Kaptain Wayne Rooney kufunga Goli la 3 katika Dakika za lala salama kwa mkwaju wa penati. Mpaka dakika 90 zinakamilika Man Utd 3-1 Preston Noth End.
Kwa matokeo hayo Manchester United Wametinga robo fainali ya kombe hilo Ambapo watakutana na Arsenal Machi 7 au 8 katika Uwanja wa Old Trafford.