MATIC AANZA MAZOEZI MAN UNITED AKISHEREHEKEA SIKU YA KUZALIWA

Kiungo mpya wa Manchester United, Nemanja Matic (kushoto) ambaye leo anasherehekea siku yake ya kuzaliwa akizungumza na mchezaji mwenzake wa zamani wa Chelsea, Juan Mata kwenye mazoezi ya Mashetani hao Wekundu leo PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

SANCHEZ ALIVYOREJEA NA MOTO WA KE ARSENAL

Nyota wa Arsenal, Alexis Sanchez akifanya mazoezi kwa bidii baada ya kujiunga na timu yake hiyo leo kufuatia mapumziko marefu zaidi aliyopewa tofauti na wenzake baada ya kuwa amekwenda kuiongoza timu yake ya taifa, Chile kwenye michuano ya Kombe la Mabara Juni mwaka huu, ambako ilishika nafasi ya pili baada ya kufungwa 1-0 na Ujerumani katika fainali PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

LIVERPOOL YAILAZA 3-0 BAYERN MUNICH UJERUMANI

Mshambuliaji Msenegal, Sadio Mane akiruka juu kushangilia baada ya kuifungia Liverpool bao la kwanza leo dakika ya saba katika mchezo wa kirafiki wa Nusu Fainali Kombe la Audi dhidi ya wenyeji, Bayern Munich Uwanja wa Allianz Arena mjini Munich. Mabao mengine ya Liverpool yamefungwa na Mohamed Salah dakika ya 34 na Daniel Sturridge dakika ya 83 PICHA ZAIDI GONGA HAPA 
 

HASSAN ISIHAKA ATUA MTIBWA SUGAR

 

MABINGWA wa zamani wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Mtibwa Sugar wameendeela kujiimarisha kuelekea msimu ujao baada ya kumsajili beki wa zamani wa Simba SC, Hassan Suleiman Isihaka.
Timu hiyo inayomilikiwa na kiwanda cha Sukari bora nchini Mtibwa Sugar kilichopo mkoani Morogoro, imefanikiwa kunasa saini ya beki huyo ambaye msimu uliopita aliichezea kwa mkopo African Lyon ya Dar es Salaam.
Hata hivyo, baada ya African Lyon kuteremka Daraja msimu uliopita, Isihaka akafikia makubaliano maalum ya kuvunja mkataba na Simba ili awe huru na hivyo kufanikiwa kujiunga na Mtibwa Sugar.
Hassan  Isihaka ametua Mtibwa Sugar ya Morogoro kutoka African Lyon alipokuwa anacheza kwa mkopo kutoka Simba, zote za Dar es Salaam 

Ujio wa beki huyo ni pendekezo la benchi la ufundi la Mtibwa Sugar linaloongozwa na Zuberi Katwila.
“Kiukweli usajili huu niliusubilia kwa hamu yote kubwa nadhani kila kocha anatamani kuwa na mchezaji huyu nadhani bahati imedondokea kwa Mtibwa Sugar , pia natoa shukrani za dhati kwa viongozi kwa kufanikisha usajili huu maana ulikua wa muhimu sana kwangu,” amesema Katwila.
Kwa upande wake. Isihaka amesema kwamba alikua anatamani kufanya kazi na 'Wana Tam Tam' kwa muda mrefu; “Nilikua natamani kufanya kazi na Mtibwa Sugar kwa muda mrefu na ninadhani nimefanikiwa kwa kuwa ni klabu kubwa na wachezaji wengi nchini wakubwa wamepita hapa,” amesem Isihaka.
Isihaka anakuwa mchezaji mpya wa saba kusajiliwa na Mtibwa Sugar dirisha hili, wengine wakiwa ni kipa Shaaban Hassan Kado, mabeki Salum Kanoni kutoka Mwadui, Hussein Idd Hante kutoka JKT Oljoro, viungo Hassan Dilunga kutoka JKT Ruvu na washambuliaji ni Riffat Khamis Msuya kutoka Ndanda FC na Salum Ramadhani Kihimbwa 'Chuji'.

DIDA ASAJILIWA AFRIKA KUSINI

 

 

 
GOLIKIPA wa kimataifa wa Tanzania, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na timu ya soka ya Chuo Kikuu cha Pretoria, inayofahamika kama Tuks FC ya Afrika Kusini.
Timu hiyo yenye maskani yake Hatfield mjini Pretoria kwa sasa inacheza Ligi Daraja la Kwanza nchini Afrika Kusini na inajaribun kuchukua wachezaji wakubwa wenye uzoefu katika jitihada za kurudi Ligi Kuu ya ABSA Afrika Kusini.
Dida anajiunga na timu hiyo baada ya kumaliza mkataba wake Yanga SC na kuamua mwenyewe kuondoka ili kwenda kusaka changamoto mpya baada ya kucheza Tanzania kwa muda mrefu.
Dida amedakia klabu zote kubwa Tanzania, kuanzia Simba, Azam FC, Mtibwa Sugar na Yanga baada ya kuibukia Manyema FC, wakati pia amewahi kucheza soka ya kulipwa Oman.
Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Tuks FC ya Ligi Daraja la Kwanza Afrika Kusini

Katika timu zote alizowahi kudakia, Dida alikuwa kipa namba moja, kasoro Simba SC pekee ambako alishindwa kumuondoka Juma Kaseja langoni.
Na ni kutokana na kiu yake ya kutaka kudaka, Dida aliamua kuondoka Simba na kwenda Mtibwa Sugar ili apate nafasi ya kucheza.
Dida aliyezaliwa mwaka 1989 Moshi, Kilimanjaro katika familia ya Mzee Bonaventure Munishi (marehemu) na mama Hilda Temu akiwa ni mtoto wa pili katika familia hiyo ya watoto wanne na ndugu zake ni Ismail, Kasija na George.
Alisoma Madenge shule ya msingi kuanzia mwaka 1996 mpaka 2002 kisha kujiunga na Makongo sekondari mwaka uliofuata lakini alisoma kwa mwezi mmoja tu na kujikita katika soka.
Dida akiwa na mshambuliaji wa zamani wa Ivory Coast, Didier Drogba baada ya mechi na Tanzania mwaka 2010
Alianza kucheza soka mwaka 1993 katika viwanja vya Temeke msikiti wa Tungi kisha alijiunga na timu ya Temeke Kids mwaka 2000 iliyokuwa chini ya Kocha Tunge na kufanya mazoezi katika viwanja vilivyokuwapo jirani ya Uwanja wa Taifa wa zamani (sehemu hiyo sasa imemegwa na Uwanja Mkuu wa Taifa).
Mwaka 2004 alisajiliwa na Coastal Union ya Tanga na kucheza Ligi daraja la kwanza, mwaka uliofuata alijiunga na timu ya Chuoni ya Zanzibar iliyokuwa ikishiriki Ligi Daraja la Kwanza visiwani humo.
Mwaka uliofuata alijiengua katika timu hiyo na kurudi Dar es Salaam na kuendelea kujifua katika viwanja vya Tungi, Temeke. Februari 2007 alijiunga na timu ya Makondeko ya Temeke na kushsiriki Ligi ya Taifa, lakini Machi mwaka huo huo alijiunga na Mkunguni ya Ilala kushiriki Ligi ya Taifa pia.
Hapo hakuka sana kwani Aprili, 2007 alijiunga na Manyema kucheza Ligi Daraja la kwanza na kufanikiwa kuipandisha timu hiyo Ligi Kuu, ndipo Simba ilipomuona na kumsajili mwezi Novemba mwaka huo huo kutokana na uwezo aliouonyesha katika timu hiyo.
Baada ya miaka miwili akaondoka Simba kwenda Mtibwa, baadaye Oman kabla ya kusajiliwa Azam FC ambako alidaka mwaka 2013 alipojiunga na Yanga. Amekuwa kipa wa timu ya taifa tangu mwaka 2009 chini ya kocha Mbrazil, Marcio Maximo kabla ya hivi karibuni kuachwa na kocha mzalendo, Salum Mayanga.

LIGI DARAJA LA KWANZA TANZANIA BARA KUANZA SEPTEMBA 16

Mambo 8 yatakayofanywa katika wiki ya Simba SC

 
Jumanne August 1, 2017 Simba SC imezindua rasmi wiki ya Simba kuelekea Simba Day August 8 ambapo imekuwa kawaida kwa Klabu hiyo kuadhimisha Siku Maalumu waliyoiita ‘Simba Day’ kila ifikapo August 8 wakati ambapo timu hiyo imeweka kambi Afrika Kusini kwa ajili ya msimu ujao.
Simba SC, mbele ya waandishi wa habari akiwepo Afisa Habari wao Haji Manara na Mshirika wao wa kibiashara CEO wa EAG Group Iman Kajula wamezindua wiki ya Simba na kutaja mambo mbalimbali yatakayofanyika.
Uzinduzi huo umefanywa na timu hiyo wakiandaa mambo 8 ambayo yatafanyika ikiwa ni pamoja na kutoa msaada kwa watoto yatima huku Simba Day, kabla ya kucheza game ya kirafiki na Rayon Sport ya Rwanda zitachezwa mechi za utangulizi za Simba Queens dhidi ya viongozi wa Simba.
VIDEO: Manara wa Simba amefunga mjadala wa Haruna Niyonzima August 1 20

Manara ;Haruna Niyonzima ni mali ya simba

 
Baada ya headlines za muda mrefu kuhusiana na club ya Simba kuhusishwa kumsajili kiungo wa kimataifa wa Rwanda aliyekuwa anaichezea Yanga Haruna Niyonzima, kwa mara ya kwanza leo August 1 2017 Simba wamekubali na kuweka wazi.
Simba kupitia mkuu wao wa idara ya habari na mawasiliano Haji Manara wametangaza rasmi kumsajili Niyonzima ambaye bado yupo kwao Rwanda akimalizia mambo yake binafsi ya kifamilia na ataungana na timu Tanzania.
“Kuhusu Juuko ni mchezaji wetu na ataungana na timu suala la kwenda Orlando hatujapata taarifa, kuhusu Haruna ni mchezaji wa Simba ukiona ndege imetua hapa na wachezaji wa Simba ujue ndani yupo Haruna au anaweza kuja mapema kabla ya timu” >>> Manara

MAN UNITED WAREJEA NYUMBANI BAADA YA KAMBI YA MAREKANI


Mshambuliaji mpya wa Manchester United, Romelu Lukaku aliyesajiliwa kwa dau la Pauni Milioni 75 kutoka Everton akisaini jezi ya shabiki wa timu hiyo baada ya kuwasili mjini Manchester leo wakitokea Marekani ambako walikwenda kuweka kambi ya kujiandaa na msimu mpya pamoja na kucheza mechi za kujipima nguvu za mashindano ya Kombe la Mabingwa wa Kimataifa PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

DAVID LUIZ KATIKA MAZOEZI YA HATARI

Beki wa Chelsea, David Luiz akifanya mazoezi ya nguvu katika gym mjini Singapore alipokuwa na timu yake kwa ziara yake ya maandalizi ya msimu mpya PICHA ZAIDI GONGA HAPA 
 
Supported by AMAGA Media services : | |
Copyright © 2015. UKURASA WA HABARI - All Rights Reserved
Templete Designed by Abdallah Magana
Proudly powered by Blogger