Baraza
zima la Madiwani pamoja na wakuu wa Idara wakiendelea na Mkutano
MKUU wa Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya,
Gulam Hussein Kiffu, amewataka Madiwani kusaidiana na Watendaji wa Kata na
Vijiji kuwahamasisha wananchi kuchangia ujenzi wa Maabala unaondelea wilayani
humo.
Wito huo aliutoa katika Mkutano wa
kwanza wa mwaka wa fedha 2014/2015 wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya
Wilaya ya Mbarali uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Maji uliopo Rujewa.
Kiffu alisema licha ya uwepo wa
kasi nzuri ya ujenzi wa Maabara katika shule za Sekondari wilayani humo ni vema
Madiwani wakaendelea kuwahamasisha Wananchi wakishirikiana na Watendaji
kuchangisha fedha za umaliziaji wa majengo hayo.
Alisema ni matumaini yake kuwa ifikapo
mwezi Novemba zoezi hilo likawa limekamilika kwa kiwango kikubwa na
kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kufanya ziara ya kukagua majengo hayo tayari
kwa kuanza kuyatumia.
Alisema uwepo wa Maabara katika shule za
Sekondari kutasaidia upatikanaji wa wataalamu wa masomo ya sayansi kutokana na
kuandaliwa kuanzia ngazi ya chini kwa vitendo hali itakayowasaidia kuwaimarisha
na kuwahamasisha wanafunzi kuyapenda masomo ya sayansi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali, Adam Kingoyi, alisema ni vema wanasiasa
wakasaidia kuhamasisha shughuli za maendeleo katika maeneo yao na sio
kukwamisha wakihofia kunyimwa kura katika uchaguzi ujao.
|
0 comments:
Post a Comment